Gari ya Tsh. 12M

Gari ya Tsh. 12M

Gari gani yakishamba hio kwani wewe ni mzee au mshamba wa vijijini? Ongera Pesa ufike 15 nunua zako Crown or Bmw uenjoy maisha achana na ivyo vigari vyakubebea nyasi spacio sibebi hata bure hata kwa lift sipandi ni mara mia nitembee
Dah[emoji2]
 
Habari wana JF
Niliwahi kuleta Uzi wa kutaka kununua gari ya Tsh. 7M lakini wengi walinishauri tapata kimeo hivyo ilibidi nijichange Kwa muda mrefu na nimefanikiwa kufikisha tsh. 12M
Naomba ushauri ni gari Gani litanifaa Kwa hiyo pesa ambalo taagiza Moja Kwa Moja kutoka japane na sio Kwa mtu.

Zingatia. Sijawahi kumiliki gari na Wala Sina elimu yeyote kuhusu Gari, sijui kuendesha, usafiri wangu ni boda yangu tu.

Binafsi nilitamani IST new model lakini mkwanja wake naona mrefu.

Wakuu ushauri wenu
Hapo kwa hiyo pesa upo vema sana. Mawili unaweza kuamua.

Unaweza kuagiza ila itabidi uongeze hela kidogo hapo ili upate IST kaliiii kutoka japani.

Lakini pia unaweza nunua ya mtu mwingine used kwa bajeti chini ya hiyo hela yaani kati ya 6.5 hadi 8 utaweza kujiokotea IST kali sana ila kwa sharti moja tu usiongee na madalali maana watakuwa na haja ya kukufilisi tu na sio kukusaidia. Usiwe na haraka sana sababu hela unayo na una uhuru wa maamuzi so take your time bro.

So wewe make a choice
 
Kwa uhakika kwa sifa hizi...
1. Ni mara yako ya kwanza kumiliki gari
2. Huna ujuzi wowote wa kumiliki magari
3. Budget yako ni 12m

Gari inayokufaa zaidi ni Toyota IST old model. Huwezi kujutia kabisa.

Naona pia umewaza kuhusu Toyota IST new model, lakini jibu unalo tayari, gharama ya kuweza kulinunua iko juu zaidi japokuwa ni gari nzuri pia. Kama hiyo ndio dream yako, na ikiwa ni suala la kufa na kupona basi inabidi uvute subira na ujipange zaidi ili ujiongeze na kufikia around 16m ili kufikia ndoto zako.
16m tokea lini IST ukaimport kwa 16 milioni au washapandisha ushuru?!
 
Gari gani yakishamba hio kwani wewe ni mzee au mshamba wa vijijini? Ongera Pesa ufike 15 nunua zako Crown or Bmw uenjoy maisha achana na ivyo vigari vyakubebea nyasi spacio sibebi hata bure hata kwa lift sipandi ni mara mia nitembee
Mfalme Betshaza alianzaga hivihivi! Tubu mkuu
 
Wakuu hivi gari za Nissan mbona hazina promo kama Toyota au Zina shida Gani?
Mfano Nissan note 2013 Hadi mkononi ni 12.5M
Hizi Huwa Zina shida Gani, nipeni muongozo wazee wa ndinga
 
Wakuu hivi gari za Nissan mbona hazina promo kama Toyota au Zina shida Gani?
Mfano Nissan note 2013 Hadi mkononi ni 12.5M
Hizi Huwa Zina shida Gani, nipeni muongozo wazee wa ndinga
Nunua iwe ya kwako ukipata Hela ununue nyingine kuuza Nako shida spea Bei imechangamka kama nn
 
Ndio ila kama una mawe nunua ukitaka kuuza unauza kwa hasara hata 3m sawa tu
Aah wapi sinunui gari ya kunipa stress na gari ni ndoto yangu ya muda mrefu kuimiliki.
Acha niendelee kujichanga zikifika 15M nichukue ki IST cha 2005 Nile misele hamu iniishe maisha yaendelee
 
View attachment 2117288
Mkuu nakushauri uendelee kujichanga uchukue hiyo Ist second generation "new model", gari ipo luxury, imetulia, inakula 18.3km/l highway na 15.3 km/l town.....kiukweli naka enjoy sana haka kandinga.[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
Habari bhachu

Hii gari naitamani sana kumiliki.
Najua ishapita miaka miwili tangu ununue. Lakin unaweza kunipa highlights tu.

Kwa makadirio, niandae kiasi gani mfukoni niweze kuagiza hii gari, hadi kuweka road. Kila kitu.
 
Ni kweli mkuu, bado nipo nako haka kagari, Nchi yetu kila unapopinduka mwaka mpya na Kodi inaongezeka....hapo nakushauri andaa kweye 21,500,000
 
Back
Top Bottom