Gari yangu ikifika speed kuanzia 100kph inakua nyepesi, inataka kutoka barabarani, ii imekaaje!

Gari yangu ikifika speed kuanzia 100kph inakua nyepesi, inataka kutoka barabarani, ii imekaaje!

Mlolongo

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2019
Posts
3,483
Reaction score
6,257
IST/Vitz/Swift/Honda Fit

Ninamiliki moja kati ya hizo babywoka.

Nachotaka kujua ni je: Gari yangu itakua na matatizo sehemu ama ndio kawaida ya hizi babywoka.

Siku za weekend demu wangu huwa anakuja kunitembelea getto (mitaa ya Ubungo Riverside).

Jioni namrudisha kwao, anaishi Bunju na dada yake. Nikifika kule tena tunakaa weeee, wanapika chakula kitamu, nakula kisha usiku ukiwa mwingi naaga narudi zangu Ubungo.

Sasa kwa kuwa muda huo wa usiku traffic jams Bagamoyo Road zinakua zimepungua, gari chache, fujo za daladala zimefifia basi huwa natembea speed sana.

Naomba niseme tu huwa naamua kuanzisha ligi ndogondogo za magari mengine. Nayapita shaaaa nafurahi kinoma.

Tatizo nikifika speed kuanzia 80 mpaka 100 naona gari inakua nyepesi kinoma, inakua kama inataka kutoka barabarani. Yaani hata kutulia kwenye lane yangu inakua kazi.

Jana kuna Nissan Murano ilinipita pale Kibo Complex. Namie nikaamua kukimbizana nayo. Fyaaaaa fyaaaa fyuuuu... Gari ikawa inataka sijui kupaaa... Aaah mwisho nikaamua nirudi tu kwenye 60 kph. Jamaa huyooo nikaenda kumkuta mataa ya mwenge.

Sasa wakuu, hii tabia ya babywoka yangu kuwa nyepesi kama karatasi, kupoteza stability na kushindwa kutulia on the road during high speed ni kwamba gari ina tatizo ama ndio wekaness ya hizi gari ndogo.

Kama ndio zilivo niambieni nijue kabisaaa kuwa natakiwa kukaza my 'a$$' nivute Subaru Forester at the helm of next year.
 
IST/Vitz/Swift/Honda Fit

Ninamiliki moja kati ya hizo babywoka.

Nachotaka kujua ni je: Gari yangu itakua na matatizo sehemu ama ndio kawaida ya hizi babywoka...
Ukisoma motion utafunguka mengi. Sio gari yako tu, hata wew ukiwa ktk speed kali unakuwa mwepesi sana, inaweza tumika nguvu ndogo tu kukubeba na kukulisha juu. Ukitaka kuongeza stability Beba weight ktk gari yako, itatitia chini,ita tulia mno. Gari ndogo nyingi huwa nyepesi ktk motion kali, pikpiki pia ukiwa unaenda speed kali unaisikia kabisa ina shake shake , Weka weight.

Speed road na ligi za kijinga zitakugalimu chief achana nazo. Siku ukija kula mzinga utaanza ku mature road. Nishakula mizinga ya kibabe zaid ya mitatu road, na nikiwa kibati 80/100 / 120. Kooote MUNGU alinipa nafasi zaidi ya kuishi, nafungua na nina paaa kiasi kwa kunako ulazima sio ligi
 
Hizo gari ulizotaja hua zinatumika kubebea vifaa na wale wachezaj wa michezo ya golf kwenye vile viwanja vyao sasa huku kwetu bongo ukiwa na hyo gari yako mtaani kwako hapo unaonekana we mwamba ,,! Hivi unajisikia ukiw sehemu wenzio wanapak SUV we una pak baby w.
 
mhhhhhhhhhhhhh.....

Kiduku lilo akiuona huu uzi utakoma!
 
Gari nyingi za mashindano ni sawa kwa umbo km hizo gari zako na zina speed kali lkn hazipai walakuhama mstari
umeshasema Baby walker hizo gari ni maalum kwa kukupeleka kwa mchumba saluni na sokoni
 
Back
Top Bottom