Gari yangu spacio old model inakula litre 1kwa km 6

samahan naomba kuuliza hv mtu anajuaje gar yake inaenda umbal flan kwa lta
 
Nazidi kupata kitu humu humu ndani... JF ktk ubota wake.
 
samahan naomba kuuliza hv mtu anajuaje gar yake inaenda umbal flan kwa lta

Kwa kupima gari imetumia lita ngapi kwa umbali gani....
  1. Jaza mafuta hadi tenki lijae...soma 'odometer' yako na hifadhi mahali! (labda tuseme odometer inasoma kilomita 125,161)
  2. Tumia gari hadi mafuta yakaribie kuisha!
  3. Nenda jaza tena mafuta hadi tenki lijae (zimeingia lita ngapi? labda tuseme ni lita 45), soma tena odometer yako hapa (tuseme itakua kilomita 125,561)
  4. Matumizi ya gari yako ni kilomita 125,561-125,161=400 gawanya kwa lita 45
Utapata 400km/45l sawa na kusema kwa wastani kila kilomita 8.9 gari ilikula lita 1 ya mafuta.

*Kupima umbali pia unaweza kuweka 0 palipoandikwa trip, kisha utajua hadi kujaza mafuta mengine ilitembea umbali upi.
 
Ilikuwa, ya kuambiwa changanya na ya kwako
 
kwa nn gari inakula mafuta?? kutakuwa sehem kuna recage kama sio basi kuna sehem kutakuwa na shida je gari yako ina miss?? je gari yako inabadili gia vizuri??je gari yako ina recage ya hews sehem yoyote ile??

gari imegawanyika sehem 3 kwanza mfumo wa hewa 2 mfumo wa mafuta 3 mfumo wa uchomaji.

mfumo wa hewa hapo kuna sensor mbali mbali kutokana na aina ya engine lkn kutokana na hiyo engine yako vitu vya kuangalia hapo ni air clener ,vaccum sensor na kubwa zaidi inayoweza kuchangia kwa tatizo lako hilo ni idle sensor.
hapo inatakiwa kuangalia hali ya gari ukiiwasha inakuwaje unaangalia nyuma.gari inatowa moshi wa aina gani au unakwenda kunusa moshi upoje??

inatakiwa ukaguwe pipe zote za hewa zisiwe zina vuja.maana nazo huchangia gari kula sana mafuta??.


mfumo wa mafuta hapo unakagua petrol filter,pump na nozel vile vile angalia pipe za kutoka kwenye tank mpaka kwenye engine maana hapo huwa kuna kuwa na pipe 3 main inayopeleka mafuta kwenye nozel hakikisha haivuji,
pipe ya return huwa inarudisha mafuta kwenye tank nayo pia hakikisha haivuji

pipe ya hewa hii huwa kwaajiri ya kupumua hulifanya kutoa gesi kwenye tank bila hivyo matanki ya gari yangekuwa yanafumuka hii pipe huwa inachomekwa kwenye charcol kenister ili ile hewa ya unyevu unyevu ya petrol iweze kuchujwa na kuwa hewa kavu then baada ya hapo huwa kuna kuwa na.valve 1 inaingia na ikiruhusiwa huingia kwenye injection curbureter so hii pipe kama itakuwa inavuja mafuta yatakuwa yanapungua sana kwa njia ya mvuke or hewa.

baada ya hapo jaribu kucheki nozel zako zinaweza kuwa zinavujisha sana mafuta.

mfumo wa uchomaji hapo jaribu kucheki plug,wire plug .

ila ukimpa fundi ni rahisi zaidi kufaham eneo lipi linashida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…