Miaka michache kabla ya utawala wa JK kufikia tamati kuliibuka swala la GAS Mtwara, kwa maneno ya Wapinzani mkataba wa Gas Mtwara ukapata pingamizi kubwa zaidi ya pingamizi zinazoonekana leo, hata kufikia wakati Jeshi likaingizwa kazini ndio mkandarasi aweze laza mabomba ya gas. Mabomba hayo leo ndio yanayopitisha Gas kwa uchache, inasemekana so far ni chini ya asilimia 15 ya uwezo wa bomba, ila gas hii ndio inayochangia 60% ya uzalishaji wa umeme Tanzania.
Yani isingekuwa haya mabomba kuna uwezekano mkubwa leo Tanesco ingeshakuwa mufilisi kutokana na matumizi ya mafuta ya diezel, kipindi unit moja ya umeme ni Sh 350 kwa bei ya Tanesco, ila ukizalisha umeme kwa mafuta ya diesel unit moja hufika Sh 700, na bei ya mafuta ilivyopanda leo, inawezekana kabisa Tanesco ingekuwa inatumia Sh 900 kuzalisha umeme inaouza Sh 350.
Watu wachache walieneza chuki kwa watu wa kusini, ikawa mtiti kweli kweli. Ila leo hii Gas hii ndio imeliokoa Shirika la Tanesco, na uchimbaji utavyoongezeka basi manufaa yatakuwa makubwa zaidi, sio tu kwa Tanesco bali hata kwenye magari na majumbani.
Leo hii tunaona mkataba wa bandari unavyopigiwa kelele, kuna vitu vingine vinaongewa kishabiki na kwa kupotoshwa kabisa, japo vichache kweli vinaleta mashaka, vitu kama bandari imeuzwa, ukomo wa mkataba, etc ni vitu vinavyoongewa kisiasa zaidi kuliko uhalisia. Mtu anakwambia anataka tukivunja mahusiano na Dubai basi mkataba uwe terminated, Hivi inawezekana vipi tumeingia mkataba na DPW wa miaka 25, wameshusha crane/lift za kutosha za kushushia makontena, then miaka miwili anaingia kiongozi mwingine anavunja mahusiano na Dubai na kuvunja mkataba na DPW, nani atalikubali hilo, na hata akilikubali, mahakama huko South Africa itaamua tofauti na tutapigwa mabiliani ya Shilingi kwenye kesi kama tunavyopigwa sasa kwenye kesi tofauti tofauti. Ikumbukwe kiini cha kesi zote hizi ni kuvunja mikataba kihuni bila sababu za msingi.
Swala la DPW kwa sasa ni swala lililotumika kuwapatia watu milage zaidi kuliko kutafuta ufumbuzi wa vipengele vichache vyenye kuleta walakini. Badala ya kujenga wachache wameamua bomoa kwa manufaa ya kwao kisiasa.
Miradi mikubwa nchini kila mara imekuwa ikipata mapingamizi mengi bila sababu za msingi. Bwawa la Nyerere lilipigwa vita na hao hao leo wanaolalamika mbona linachelewa washa umeme, SGR hii ilipigwa vita na hao hao leo wanaouliza mbona vichwa vya treni vinachelewa wakati wanajua fika Covid-19 ndio chanzo cha uzalishaji duniani kudorola, yapo makampuni ya uzalishaji magari yameshindwa timiza malengo yake na mengine kuuzwa kabisa kutokana na uzalishaji duni ulioletwa na Covid-19 plus vita ukraine.
Tesla Cybertruck ilikuwa iingie sokoni 2021, ila leo hii itaingia barabarani 2024, yote hiyo ni Covid-19 plus Ukraine war, TRC ni nani hata vichwa vya Treni vifike kwa wakati wakati dunia nzima imesimama.
Sitetei CCM, Sipondi Upanzani, ila nataka tu ujue kuna watu wanapotosha sana uhalisia wa mambo ulivyo kwa manufaa yao binafsi.
Kwaheri.