GAS Mtwara vs Bandari Tanzania

GAS Mtwara vs Bandari Tanzania

Miaka michache kabla ya utawala wa JK kufikia tamati kuliibuka swala la GAS Mtwara, kwa maneno ya Wapinzani mkataba wa Gas Mtwara ukapata pingamizi kubwa zaidi ya pingamizi zinazoonekana leo, hata kufikia wakati Jeshi likaingizwa kazini ndio mkandarasi aweze laza mabomba ya gas. Mabomba hayo leo ndio yanayopitisha Gas kwa uchache, inasemekana so far ni chini ya asilimia 15 ya uwezo wa bomba, ila gas hii ndio inayochangia 60% ya uzalishaji wa umeme Tanzania.

Yani isingekuwa haya mabomba kuna uwezekano mkubwa leo Tanesco ingeshakuwa mufilisi kutokana na matumizi ya mafuta ya diezel, kipindi unit moja ya umeme ni Sh 350 kwa bei ya Tanesco, ila ukizalisha umeme kwa mafuta ya diesel unit moja hufika Sh 700, na bei ya mafuta ilivyopanda leo, inawezekana kabisa Tanesco ingekuwa inatumia Sh 900 kuzalisha umeme inaouza Sh 350.

Watu wachache walieneza chuki kwa watu wa kusini, ikawa mtiti kweli kweli. Ila leo hii Gas hii ndio imeliokoa Shirika la Tanesco, na uchimbaji utavyoongezeka basi manufaa yatakuwa makubwa zaidi, sio tu kwa Tanesco bali hata kwenye magari na majumbani.

Leo hii tunaona mkataba wa bandari unavyopigiwa kelele, kuna vitu vingine vinaongewa kishabiki na kwa kupotoshwa kabisa, japo vichache kweli vinaleta mashaka, vitu kama bandari imeuzwa, ukomo wa mkataba, etc ni vitu vinavyoongewa kisiasa zaidi kuliko uhalisia. Mtu anakwambia anataka tukivunja mahusiano na Dubai basi mkataba uwe terminated, Hivi inawezekana vipi tumeingia mkataba na DPW wa miaka 25, wameshusha crane/lift za kutosha za kushushia makontena, then miaka miwili anaingia kiongozi mwingine anavunja mahusiano na Dubai na kuvunja mkataba na DPW, nani atalikubali hilo, na hata akilikubali, mahakama huko South Africa itaamua tofauti na tutapigwa mabiliani ya Shilingi kwenye kesi kama tunavyopigwa sasa kwenye kesi tofauti tofauti. Ikumbukwe kiini cha kesi zote hizi ni kuvunja mikataba kihuni bila sababu za msingi.

Swala la DPW kwa sasa ni swala lililotumika kuwapatia watu milage zaidi kuliko kutafuta ufumbuzi wa vipengele vichache vyenye kuleta walakini. Badala ya kujenga wachache wameamua bomoa kwa manufaa ya kwao kisiasa.

Miradi mikubwa nchini kila mara imekuwa ikipata mapingamizi mengi bila sababu za msingi. Bwawa la Nyerere lilipigwa vita na hao hao leo wanaolalamika mbona linachelewa washa umeme, SGR hii ilipigwa vita na hao hao leo wanaouliza mbona vichwa vya treni vinachelewa wakati wanajua fika Covid-19 ndio chanzo cha uzalishaji duniani kudorola, yapo makampuni ya uzalishaji magari yameshindwa timiza malengo yake na mengine kuuzwa kabisa kutokana na uzalishaji duni ulioletwa na Covid-19 plus vita ukraine.

Tesla Cybertruck ilikuwa iingie sokoni 2021, ila leo hii itaingia barabarani 2024, yote hiyo ni Covid-19 plus Ukraine war, TRC ni nani hata vichwa vya Treni vifike kwa wakati wakati dunia nzima imesimama.

Sitetei CCM, Sipondi Upanzani, ila nataka tu ujue kuna watu wanapotosha sana uhalisia wa mambo ulivyo kwa manufaa yao binafsi.

Kwaheri.
Makuwadi wa soko huria kazini.
 
Naamini tupo mtumbwi mmoja, na mtumbwi wetu sio ule wa vibwengo anaousema Prof. Tibaijuka.
Nachoongelea hapa ni upotoshwaji wa wazi kabisa unaofanywa na wapinga mkataba. Sijabisha kwamba kuna vifungu vina walakini, ila vifungu vingi vinatumika kupotosha, mfano mmoja ni kifungu cha kuuza bandari. Kwajinsi mkataba ulivyo hakuna mahala pameandikwa au maanisha bandari imeuzwa, ila leo watu wanakimbia nchi nzima wakisema bandari imeuzwa.
Upo sawa mkuu, ila inatubidi tuelewe kwa kina nature ya mkataba tusiwe wavivu.
 
Mama asonge mbele asitishwe na yeyote.. Kwenye suala la maendeleo kuna watu watakukatisha tamaa ila songa.. Baadae hao hao watakusifia.. Ngoja bwawa la umeme lianze kutoa umeme utasikia wanashangaa

Kweli
 
last paragraph author anasema

sasa mwandishi mwenyewe wa West Africa, utaamua mwenyewe unachagua habari ya West Africa au The Citizen ya hapa hapa Bongo.
2018 umeitaja, iko wapi hapo?

Aidan Barlow ni wa West Africa?
 
2018 umeitaja, iko wapi hapo?

Aidan Barlow ni wa West Africa?
2018 nimeipata ndani ya hiyo article, kwa research aliyoifanya 2018, namna Mtwara ilivyodorora tofauti na matarajio ya wana Mtwara wenyewe.

The anticipation​

In Mtwara in 2018, I interviewed a variety of people, ranging from local business leaders, politicians and community leaders to villagers and people who used to work in the supply sector to the gas industry, about how development had been influenced by the gas sector.
 
Kwa hiyo ndiyo aliishia hapo? Umeona tarehe makala ilipochapishwa?

Na unasemaje huyu ni mtu wa West Africa?
 
Article imekaa kitapeli ki West Africa, ushaona wapi mwandishi ana article moja tu ndio hiyo hiyo, achana na reference za vichochoroni.
 
Ana article ngapi kwenye huo mtandao?

Hata akiwa na moja tu, that is logical non sequitur.

Yani kujamba ujambe wewe, lawama unipe mimi?

Umesema article ya West Africa, nimekuuliza ushahidi, umethibitisha kwamba umezusha tu.

I rest my case.
 
Miaka michache kabla ya utawala wa JK kufikia tamati kuliibuka swala la GAS Mtwara, kwa maneno ya Wapinzani mkataba wa Gas Mtwara ukapata pingamizi kubwa zaidi ya pingamizi zinazoonekana leo, hata kufikia wakati Jeshi likaingizwa kazini ndio mkandarasi aweze laza mabomba ya gas. Mabomba hayo leo ndio yanayopitisha Gas kwa uchache, inasemekana so far ni chini ya asilimia 15 ya uwezo wa bomba, ila gas hii ndio inayochangia 60% ya uzalishaji wa umeme Tanzania.

Yani isingekuwa haya mabomba kuna uwezekano mkubwa leo Tanesco ingeshakuwa mufilisi kutokana na matumizi ya mafuta ya diezel, kipindi unit moja ya umeme ni Sh 350 kwa bei ya Tanesco, ila ukizalisha umeme kwa mafuta ya diesel unit moja hufika Sh 700, na bei ya mafuta ilivyopanda leo, inawezekana kabisa Tanesco ingekuwa inatumia Sh 900 kuzalisha umeme inaouza Sh 350.

Watu wachache walieneza chuki kwa watu wa kusini, ikawa mtiti kweli kweli. Ila leo hii Gas hii ndio imeliokoa Shirika la Tanesco, na uchimbaji utavyoongezeka basi manufaa yatakuwa makubwa zaidi, sio tu kwa Tanesco bali hata kwenye magari na majumbani.

Leo hii tunaona mkataba wa bandari unavyopigiwa kelele, kuna vitu vingine vinaongewa kishabiki na kwa kupotoshwa kabisa, japo vichache kweli vinaleta mashaka, vitu kama bandari imeuzwa, ukomo wa mkataba, etc ni vitu vinavyoongewa kisiasa zaidi kuliko uhalisia. Mtu anakwambia anataka tukivunja mahusiano na Dubai basi mkataba uwe terminated, Hivi inawezekana vipi tumeingia mkataba na DPW wa miaka 25, wameshusha crane/lift za kutosha za kushushia makontena, then miaka miwili anaingia kiongozi mwingine anavunja mahusiano na Dubai na kuvunja mkataba na DPW, nani atalikubali hilo, na hata akilikubali, mahakama huko South Africa itaamua tofauti na tutapigwa mabiliani ya Shilingi kwenye kesi kama tunavyopigwa sasa kwenye kesi tofauti tofauti. Ikumbukwe kiini cha kesi zote hizi ni kuvunja mikataba kihuni bila sababu za msingi.

Swala la DPW kwa sasa ni swala lililotumika kuwapatia watu milage zaidi kuliko kutafuta ufumbuzi wa vipengele vichache vyenye kuleta walakini. Badala ya kujenga wachache wameamua bomoa kwa manufaa ya kwao kisiasa.

Miradi mikubwa nchini kila mara imekuwa ikipata mapingamizi mengi bila sababu za msingi. Bwawa la Nyerere lilipigwa vita na hao hao leo wanaolalamika mbona linachelewa washa umeme, SGR hii ilipigwa vita na hao hao leo wanaouliza mbona vichwa vya treni vinachelewa wakati wanajua fika Covid-19 ndio chanzo cha uzalishaji duniani kudorola, yapo makampuni ya uzalishaji magari yameshindwa timiza malengo yake na mengine kuuzwa kabisa kutokana na uzalishaji duni ulioletwa na Covid-19 plus vita ukraine.

Tesla Cybertruck ilikuwa iingie sokoni 2021, ila leo hii itaingia barabarani 2024, yote hiyo ni Covid-19 plus Ukraine war, TRC ni nani hata vichwa vya Treni vifike kwa wakati wakati dunia nzima imesimama.

Sitetei CCM, Sipondi Upanzani, ila nataka tu ujue kuna watu wanapotosha sana uhalisia wa mambo ulivyo kwa manufaa yao binafsi.

Kwaheri.
Uongo mtupu..

Nilichokuja kugunduaa mikataba asilima 95 inakuwaga ni ya ovyooo sanaa sema ni vilee tu huwa haivujiii...!! no wonder umeme wa gas imebaki kuwa maneno matupuuu na siasaa... gas ukute inasafirii kwenda nje daily.
 
Mfanyabiashara yoyote anapotaka wekeza kwako lazima aweke vipengele vitavyomlinda kwa investment anayofanya. Hata wewe leo ukiona kiwanja Masaki/Mikocheni ukataka fanya investment, lazima utaweka masharti yatayombana mmiliki ili siku asije kengeuka akasema toa maghorofa yako niachie kiwanja changu. Sasa mmbongo akiwekewa masharti anasema unyonywaji.
 
yapo masharti kweli lakini sio ya kusema umiliki bandari mileleee...!! kuna masharti inabdi uyapimee lasivyoo leo sisi tusingekuwa wamiliki wa hii ardhi maana kila sehemu pangemilikishwa kitamaaa.
 
hapo ndio kuna upotoshwaji wenyewe hulipo, hakuna kipande cha bandari kilichouzwa, bandari imekodishwa kama ilivyokodishwa sasa kwa TICTS.
 
Mama asonge mbele asitishwe na yeyote.. Kwenye suala la maendeleo **** watu watakukatisha tamaa ila songa.. Baadae hao hao watakusifia.. Ngoja bwawa la umeme lianze kutoa umeme utasikia wanashangaa
Hujaona ripoti ya Tanesco jana kuwa bwawa likianza kufanya kazi bei ya umeme itaongezeka per unit?
 
Back
Top Bottom