Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Gati linaloelea majini lililojengwa Gaza na Marekani kupitishia misaada kabla kufanya kazi yake limeshakumbwa na matatizo mara kadhaa na mwishowe limebomoka kutokana na upepo mkali.
Habari zinazoendelea kutolewa ni kuwa dude lote limeanza kuzama na haitokuwa rahisi kuliokoa.
Muda mfupi kabla kukamilika wajenzi ilibidi wahamie Haifa ndani ya Israel ili kuendelea kuunganisha vifaa vyake baada ya kukumbwa na hali mbaya ya hewa.
Ujenzi wa bandari hiyo tangu hapo awali haukuwa na umuhimu wakati malori yalikuwa yamejazana mpaka wa Rafah yakisubiri kuingia Gaza kwa njia ya kawaida ya ardhini.