Investigation Unit
JF-Expert Member
- Nov 26, 2023
- 216
- 301
===
Billionaire wa Kihindi na tajiri namba mbili barani Asia Mr Gautam Adani anayetajwa pia kuwa ni miongoni mwamatajiri kumi ( 10 ) duniani anakabiliwa na tuhuma za kuahidi kutoa rushwa ya kiasi cha US$ 250M zaidi ya TZS 650bn ili apate kazi na Mikopo toka kwa mabanki na Wawekezaji wenzake kibiashara.
Billionaire Gautam Adani anatajwa kumiliki ukwasi wa zaidi ya US$ 85.5bn zaidi ya TZS 222.3trilioni ambazo ni zaidi ya Uchumi wote wa nchi ya TANZANIA wenye wasi wasi nae kuhusu uwezo wa Kiuchumi naomba waondoe hofu.
Mtakumbuka billionaire huyu hivi karibuni alionesha nia ya kuwekeza nchini Marekani kiasi cha US$ 10bn zaidi ya TZS 26 Trilioni kwenye sekta ya nishati akiahidi kutoa ajira za moja kwa moja kwa wamarekani zaidi ya 15,000 akitaraji kupata faida ya karibu US$2bn zaidi ya TZS 5.2trlioni ndani ya miaka 20 ijayo.
Billionaire huyo kwa kupita kampuni yake Adan Green Energy Ltd pamoja na kampuni ya Gridworks Development Partners LLP toka Uingereza kwa nyakati tofauti tofauti wameonesha nia ya kutaka kuwekeza kwenye mradi wa kusafirisha na kusambaza Umeme kwa gharama ya zaidi ya TZS 3.3Trilioni ikiwa ni baada ya Tanzania kuwa na Umeme wa ziada wa zaidi ya 600MW hii ni baada ya bwawa la Mwl Nyerere (JNHPP) kukamilika na kuanza kufua umeme wa zaidi ya 2,100MW na kuziba nakisi ya umeme iliyokuwepo kwa miongo mingi na hivyo kuilazimu Tanzania kuuza umeme nje ya nchi.
Haya ni maoni yangu
1. Tuhuma hizi kwa Serikali ya Tanzania ni ama zimewahi ama hazina msingi wowote kwakuwa billionaire Gautam Adani hana mkataba wowote na Serikali ya Tanzania japo ameonesha nia ya kuwekeza kwa kutumia Sheria , kanuni na taratibu za PPPC.
2. Hata hivyo kinachomsibu Gautam Adani Kwa sasa ni tuhuma tu tena za Upande mmoja na kwa kuzingatia dunia hii ya mnyukano wa vita za Kiuchumi tusiende mbio kwenye lawama badala yake tujiuluze kwanini Marekani yenyewe imruhusu billionaire Gautam Adani awekeze kiasi Cha US$ 10bn na hivyo kutoa ajira zaidi ya 15,000 kwa wamarekani?
3. Hata hivyo, hakuna mahali Serikali ya Tanzania wala Mkurugenzi wa PPP Bw David Kafulila wamemtetea billionaire Gautam Adani au mwekezaji mwingine yeyote.
4. Kwa msiofahamu kazi mojawapo ya PPPC ni kuueleza umma wa Tanzania ( Public ) kuhusu uwekezaji na wawekezaji wenye nia ya kuwekeza kwenye PPP kwa kuzingatia zaidi masilahi mapana ya Taifa la Tanzania.
5. Lazima tufahamu kwanini PPPC anafanya hivi, lengo na nia ni kuufanya Umma ( Public) uelewe kila kitu tangu mwanzo kabisa wa mradi hasa kwenye hatua ya mwekezaji kuonesha nia badala ya Umma kuja kuletewa mkataba ulosainiwa bila kujua mchakato wa uwekezaji huo ulianza lini na kwa namna gani na masilahi kwa Taifa ni yepi hivyo kupoteza maana ya neno Public-Private
Tukumbuke Transparency ndio nguzo kuu katika ndoa yoyote ile ya PPP na faida yake ni hii Leo Watanzania wanamjadili Adani nje ndani ni kwa sababu wameshirikishwa mapema na kwa uwazi kabisa juu ya nia yake hiyo.
Pia soma: Bilionea Gautam Adani ambaye Kafulila anataka kumpa shirika la TANESCO ashitakiwa kwa utapeli huko Marekani
search.app
search.app
#SAMIAMITANOTENA