Gautam Adani na kashfa ya rushwa Marekani: Je, ni nini hatma ya TANESCO na PPP ya David Kafulila, tenda apewe au atoswe?

Afrika tunalo tatizo la kutumika kwa ajili ya maslahi ya wakubwa fulani. DPW alipingwa na kanisa na unaweza kudhani kuwa kanisa ni safi na takatifu kumbe lilitumika kwa maslahi ya makundi makubwa ya wafanyabiashara.

Dangote anapigwa vita katika uwekezaji wa sekta ya mafuta anaoufanya kwao Nigeria, ni dunia iliyojaa kila aina ya umafia.
Usipotoshe.
Kinacho pingwa ni ufisadi. Miradi inayo ingiwa gizani kwa kuficha kila kitu ili madudu yasionekane.
Wewe mwenyewe humu ulisha sema na kumhimiza Samia kila kitu afanye gizani, watu wasijue kinacho endelea!

Sasa mnageuza stori na kulalamikia watu na makundi yanayo pigania maslahi ya wananchi.

Sasa wewe tueleze, ni waTanzania wangapi wanajuwa kwamba gesi ya Mtwara (Ntor) Samia alikwisha wagawia Omani; ni waTanzania wangapi wanajuwa Adani huyo huyo alisha pewa mradi wa kuzalisha umeme wa makaa ya mawe. Huko bandarini, nani anaye juwa ni makubaliano gani huyo Adani aliingia nayo na serikali yetu.
Kila kitu mnafanya gizani, halafu mnawaona waTanzania kama majuha!
 
Hata top 10 hayupo. Acha ujinga
IMG-20241121-WA0087.jpg
 
Ukiamua kusikiliza umbea na kuuamini hilo ni tatizo lako binafsi. Haswa ukiwa unaongozwa na chuki kwa SSH. Hakuna wa kukuzuia kuziamini stori za kwenye viti virefu vya Bar.
 
===
Billionaire wa Kihindi na tajiri namba mbili barani Asia Mr Gautam Adani anayetajwa pia kuwa ni miongoni mwamatajiri kumi ( 10 ) duniani anakabiliwa na tuhuma za kuahidi kutoa rushwa ya kiasi cha US$ 250M zaidi ya TZS 650bn ili apate kazi na Mikopo toka kwa mabanki na Wawekezaji wenzake kibiashara.

Billionaire Gautam Adani anatajwa kumiliki ukwasi wa zaidi ya US$ 85.5bn zaidi ya TZS 222.3trilioni ambazo ni zaidi ya Uchumi wote wa nchi ya TANZANIA wenye wasi wasi nae kuhusu uwezo wa Kiuchumi naomba waondoe hofu.

Mtakumbuka billionaire huyu hivi karibuni alionesha nia ya kuwekeza nchini Marekani kiasi cha US$ 10bn zaidi ya TZS 26 Trilioni kwenye sekta ya nishati akiahidi kutoa ajira za moja kwa moja kwa wamarekani zaidi ya 15,000 akitaraji kupata faida ya karibu US$2bn zaidi ya TZS 5.2trlioni ndani ya miaka 20 ijayo.

Billionaire huyo kwa kupita kampuni yake Adan Green Energy Ltd pamoja na kampuni ya Gridworks Development Partners LLP toka Uingereza kwa nyakati tofauti tofauti wameonesha nia ya kutaka kuwekeza kwenye mradi wa kusafirisha na kusambaza Umeme kwa gharama ya zaidi ya TZS 3.3Trilioni ikiwa ni baada ya Tanzania kuwa na Umeme wa ziada wa zaidi ya 600MW hii ni baada ya bwawa la Mwl Nyerere (JNHPP) kukamilika na kuanza kufua umeme wa zaidi ya 2,100MW na kuziba nakisi ya umeme iliyokuwepo kwa miongo mingi na hivyo kuilazimu Tanzania kuuza umeme nje ya nchi.
Kufuatia kashfa hii ya kibiasha ya makampuni ya billionaire Gautam Adani na yanayoendelea katika Mitandao ya Kijamii hasa jukwaa hili na vyombo mablimbali vya habari vya ndani na nje ya Tanzania hasa kwa kuishambulia Serikali ya TANZANIA na watendaji wake,

Haya ni maoni yangu,

1. Tuhuma hizi kwa Serikali ya Tanzania ni ama zimewahi ama hazina msingi wowote kwakuwa billionaire Gautam Adani hana mkataba wowote na Serikali ya Tanzania japo ameonesha nia ya kuwekeza kwa kutumia Sheria , kanuni na taratibu za PPPC.

2. Hata hivyo kinachomsibu Gautam Adani Kwa sasa ni tuhuma tu tena za Upande mmoja na kwa kuzingatia dunia hii ya mnyukano wa vita za Kiuchumi tusiende mbio kwenye lawama badala yake tujiuluze kwanini Marekani yenyewe imruhusu billionaire Gautam Adani awekeze kiasi Cha US$ 10bn na hivyo kutoa ajira zaidi ya 15,000 kwa wamarekani?

3. Hata hivyo, hakuna mahali Serikali ya Tanzania wala Mkurugenzi wa PPP Bw David Kafulila wamemtetea billionaire Gautam Adani au mwekezaji mwingine yeyote.

4. Kwa msiofahamu kazi mojawapo ya PPPC ni kuueleza umma wa Tanzania ( Public ) kuhusu uwekezaji na wawekezaji wenye nia ya kuwekeza kwenye PPP kwa kuzingatia zaidi masilahi mapana ya Taifa la Tanzania.

5. Lazima tufahamu kwanini PPPC anafanya hivi, lengo na nia ni kuufanya Umma ( Public) uelewe kila kitu tangu mwanzo kabisa wa mradi hasa kwenye hatua ya mwekezaji kuonesha nia badala ya Umma kuja kuletewa mkataba ulosainiwa bila kujua mchakato wa uwekezaji huo ulianza lini na kwa namna gani na masilahi kwa Taifa ni yepi hivyo kupoteza maana ya neno Public-Private

Tukumbuke Transparency ndio nguzo kuu katika ndoa yoyote ile ya PPP na faida yake ni hii Leo Watanzania wanamjadili Adani nje ndani ni kwa sababu wameshirikishwa mapema na kwa uwazi kabisa juu ya nia yake hiyo.

Pia soma Bilionea Gautam Adani ambaye Kafulila anataka kumpa shirika la TANESCO ashitakiwa kwa utapeli huko Marekani

#SAMIAMITANOTENA
Pigisha kura mkuu
 
Kuna mpiga debe mmoja maarufu atasema Marekani wana wivu naye
 
Ukiamua kusikiliza umbea na kuuamini hilo ni tatizo lako binafsi. Haswa ukiwa unaongozwa na chuki kwa SSH. Hakuna wa kukuzuia kuziamini stori za kwenye viti virefu vya Bar.
Nilisha kueleza mara nyingi tu humu. Kama hiyo unayo ieleza kuwa ni "kuongozwa na chuki" ni kuhusu kuchukia yanayo fanyiwa taifa letu, usihangaike kabisa juu ya hilo. Nina chuki kubwa sana juu yake.

Tueleze "umbea" ni upi katika maswala yanayo fanywa na Samia. Hiyo miradi niliyo orodhesha hapo haipo? Umbea uko wapi?
Na elewa, kiongozi anapo ruhusu kufanya siri katika maswala ya wananchi wake, huyo ndiye "mmbea" mwenyewe. Samia ni kiongozi fisadi, asiye kuwa na aibu kabisa wala kujutia hali hiyo.
 
Back
Top Bottom