Gautam Adani na kashfa ya rushwa Marekani: Je, ni nini hatma ya TANESCO na PPP ya David Kafulila, tenda apewe au atoswe?

Teknolojia wanayo na viongozi wetu wanazo sababu za kuitaji utaalam wao. Elimu ya juu hupandisha thamani ya yule aliyonayo.

Mojawapo ya kipengele cha mkataba wa DPW pale bandarini ni kuwapa elimu wafanyakazi wazalendo. Tunapiga kelele humu jamvini lakini tija yetu ya kitaifa ni ndogo sana na hatuna ujanja kwa sasa bila ya kuingia ubia na hao wenye uwezo kutuzidi ambao kwa hasira zetu tunaona kama vile wanakuja kutuibia.

Dunia ya sasa haina huruma hata kidogo, usipoweza wewe mwenyewe kuzalisha ziada watakuja wenye teknolojia kufanya kazi ya kuzalisha na hawataondoka bure bure tu.
 
[emoji57]samia mitano tena ya nyokwe[emoji57][emoji57]
 
Nakuelewa sana mkuu unafafanua vema sana
 

Hivi hiyo kazi ya kuendesha kitengo cha kontena pale bandarini, hiyo tenda ilitangazwa au ndio alipewa kwa njia anazotuhumiwa nazo?
 
Wakisha kula 10%, hata tulalamike, tupige yowe, tujadili, tuseme, watapewa tenda hata mkataba uwe mbovu kama pakacha!
Chukuwachakomapema ni hatari kwa maisha ya Mtanzania!
 
Sipati picha, kafulia na tumbo lake mishuzi, insvyomtoka!!!
 
Kafulila atakuja kumchomesha Mwigulu
Sasa Mwigulu anahusikaje kwenye PPP?
Huyu Adani huko Gate 2 alipewa na Kafulila?

Kinachoendelea kwa ADANI ni vita vya Kiuchumi na makampuni makubwa ya kibiashara ya Marekani,

Mtu mwenye Uchumi zaidi ya Uchumi wote wa TANZANIA unapomzungumzia lazima uwe na nidhamu.
 
Mwigulu bears overall political responsibility kwa Wizara, hawa akina Adan ni watu ambao Kafulila kila siku anawaita waje, kumbe Kafulila amenusa kwamba wa naweza kutoa rushwa ya dola milioni Mia mbili hamsini, na yeye atapata mgao
 
Mkuu mpaka unakuja kutuuliza huku,huenda Adan alishapewa mkataba na kusaini kimyakimya muda! DP World walisaini mkataba muda kabla mambo hayajawekwa hadharani.
Tuko tayari kwa lo lote!
 

Rushwa ni sera Muhimu ya Ccm, njemba inahonga USA - NY, Ccm wanaiachaje?
 
Kutoa rushwa inatakiwa kuwa least of your problem, hiyo tsh 3.3 inalipwaje na madhara yake kwenye bei ya umeme.

We endelea kushabikia hadithi za Kafulila kama unadhani huo uwekezaji hautakuwa na madhara kwenye bei ya umeme.

Wao wenyewe unadhani wanajali madhara kwa jamii muhimu kwao ni ‘kickbacks’ za kuwatajirisha.
 
Walishasema bei ya umeme lazima ipande😂
 
Kama ana nia kweli tomtose ila kama mkataba umesainiwa TUTASHITAKIWA MIGAB kama TAL anavyotuonyaga
 
IPTL nyingine inaandaliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…