Gavana wa BoT: Deni la Taifa ni Tsh Trilioni 100, linazidi kukua japo bado linahimilika

Gavana wa BoT: Deni la Taifa ni Tsh Trilioni 100, linazidi kukua japo bado linahimilika

Wakuu,

Gavana wa Benki kuu ya Tanzania (BOT) Emmanuel Tutuba akiwa anazungumza kwenye mahojiano maalum na mwandishi wa BBC Florian Kaijage amekiri kuwa deni la taifa hilo linazidi kukua ila bado lipo chini ya ukomo wa uwiano wa deni la taifa na pato la taifa unaokubalika kimataifa wa asilimia 55%.

‘’Kwa mwaka wa 2024 deni letu la taifa la takriban shillingi trilioni 100, lipo katika uwiano wa takriban asilimia 44% ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 55%unaokubalika kimataifa’’

‘’Deni letu ni himilifu kwa muda mfupi wa kati na mrefu na lipo ndani ya viwango vinavyokubalika kimataifa.’’


Bado 9% tufike kwenye ceiling na still tunasema ni himilivu kwa hiyo asilimia kidogo iliyobaki ? Na je basisi yakukopa nikiasi gani ?
 
Tunaweza pia kusema deni linahimilika kama Mungu ataendelea kutupa neema ya kutopatikana na majanga makubwa kama njaa, vita matetemeko na magonjwa nk.Majanga hayana uhimilivu.Tukumbuke vita vya kagera tuliambiwa tufunge mikanda mpaka sasa mikanda imekaza.Hivyo serkali iwe na akiba ya busara isingoje ifike 55% ya uhimilifu kwa kuwa hatuwezi kujua impending risks dhidi yetu
 
Bado trillion 25 tufike asilimia 55% ya kiwango cha mwisho kukopa

Duuhhh hii hatari sana
 
Back
Top Bottom