Gavana wa BoT: Deni la Taifa ni Tsh Trilioni 100, linazidi kukua japo bado linahimilika

Gavana wa BoT: Deni la Taifa ni Tsh Trilioni 100, linazidi kukua japo bado linahimilika

Ukomo unawekwa na Nchi yenyewe unaweza hamishwa kutoka 55% Hadi 70% .

Mwisho Nchi zote zilizoendelea Zina madeni over 75-120 % of GDP
Ndiyo alivyosema Gavana? Au wewe ndiyo Gavana? Kama ni wewe,kwanini BBC umeleta mkanganyiko ujatoa haya maelezo.
 
Aibu kubwa sana kwa nchi yetu kusema deni himilivu ndo sifa hiyo ,utawala huu umefeli sana ,sana,tu raslimali zetu zote tunashindwa Nini??? Nchi ili iendelee inahitaji uongozi Bora sio machawa ,sifa za kijinga kila Kona ,hovyoo .tumechoka sifa za machawa kwa mama 🐸🐸🐸🐸🐸🐸🐸📢📢📢📢📢📢
Kabisa mkuu, hayo masifa hayatakiwi kikubwa ni uwajibikaji
 
‘’Kwa mwaka wa 2024 deni letu la taifa la takriban shillingi trilioni 100, lipo katika uwiano wa takriban asilimia 44% ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 55%unaokubalika kimataifa’’
Kwa hiyo tunatakiwa tukope kiasi gani ili tufike hiyo 55%?
 
Wakuu,

Gavana wa Benki kuu ya Tanzania (BOT) Emmanuel Tutuba akiwa anazungumza kwenye mahojiano maalum na mwandishi wa BBC Florian Kaijage amekiri kuwa deni la taifa hilo linazidi kukua ila bado lipo chini ya ukomo wa uwiano wa deni la taifa na pato la taifa unaokubalika kimataifa wa asilimia 55%.

‘’Kwa mwaka wa 2024 deni letu la taifa la takriban shillingi trilioni 100, lipo katika uwiano wa takriban asilimia 44% ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 55%unaokubalika kimataifa’’

‘’Deni letu ni himilifu kwa muda mfupi wa kati na mrefu na lipo ndani ya viwango vinavyokubalika kimataifa.’’

kmmk zenu wanasiasa
 
Amelikuta likiwa asilimia ngapi?
Alikuta deni likiwa 60 T, ambayo ni cumulative kwa awamu zote kabla yake.
Kwa miaka yake 4 tu ametisha mno..

Alipoingia madarakani hayati Rais John Magufuli, deni la taifa lilikuwa ni Shilingi 35 trilioni, kwa mujibu wa taarifa rasmi za Bunge la Tanzania.

Mwezi Aprili 2018 deni lilifikia Shilingi 49.9 trilioni, kwa mujibu wa Bajeti ya serikali iliyosomwa Bungeni. Mwaka mmoja baadae (Aprili 2019) deni la taifa likafika Shilingi 51.03 trilioni. Deni halikupungua. Likaendelea kukua na kufikia Shilingi 60.7 trilioni mwezi Aprili 2021.

Kwa nini deni la taifa linaendelea kuongezeka nchini Tanzania? - BBC News Swahili Kwa nini deni la taifa linaendelea kuongezeka nchini Tanzania? - BBC News Swahili
 
Wakuu,

Gavana wa Benki kuu ya Tanzania (BOT) Emmanuel Tutuba akiwa anazungumza kwenye mahojiano maalum na mwandishi wa BBC Florian Kaijage amekiri kuwa deni la taifa hilo linazidi kukua ila bado lipo chini ya ukomo wa uwiano wa deni la taifa na pato la taifa unaokubalika kimataifa wa asilimia 55%.

‘’Kwa mwaka wa 2024 deni letu la taifa la takriban shillingi trilioni 100, lipo katika uwiano wa takriban asilimia 44% ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 55%unaokubalika kimataifa’’

‘’Deni letu ni himilifu kwa muda mfupi wa kati na mrefu na lipo ndani ya viwango vinavyokubalika kimataifa.’’

Duuh, eti linahimilika? Yaani upigaji unaendelea>
 
Back
Top Bottom