- Thread starter
- #41
Mimi ndo niliuliza ni kigezo gani walifikia kutoa gawio la Tshs.36 kwa hisa. Pili, natumaini idadi ya Wakurugenzi ni kama 10 na katika taarifa watalipwa kama Tshs.965,0000,000 kwa mwaka na hivyo kila Mkurugenzi atalipwa Tshs.96,500,000 kwa mwaka na hiyo ni nje ya gharama ya safari na inawezekana wanalipwa na malazi kama complimentary na halafu ulinganishe Tshs.36 kwa hisa moja. Pili, ni kwanini ajenda ya malipo ya Wakurugenzi huletwa tu kama taarifa na kupitishwa bila majadiliano. Wanahisa wanatakiwa waelezwe kigezo cha malipo hayo. Tatu, kwa nini vikao vya Wanahisa kusiwe kwa mzunguko?. Mfano leo Arusha, Kesho Mbeya, Kesho kutwa Mwanza nk. Nawashauri Wanahisa wenzangu tusiwe watu wa ndiyooooo tuwe tunauliza maswali na kudadisi taarifa nzima katika vikao vyetu.