Gawio la hisa za CRDB

Gawio la hisa za CRDB

Wenye hisa tuna haki ya kuuliza kwanini gawio lao ni kiduchu namna hiyo huku wakurugenzi wa hiyo benki wanapata mafao makubwa!! Kama benki ikipunguza gharama zake za uedeshaji ambazo ni dhahiri kuwa ni kubwa faida ya benki itakuwa ni kubwa na wanahisa tunastahiri kupata gawio kubwa kidogo. Itakuwa busara kama management watatoa maelezo ya maswali yanayoulizwa na wanahisa ambao hatukupata nafasi ya kuwa huko Arusha.
Justification ya kulipa shs. 36 per share kutokana na faida kubwa ambayo benki imetengeneza! Nini dividend policy ya CRDB?
Tafuta EPS(Earning per share) kwa hisa za Nmb vs Crdb then utapata majibu
 
CRDB kuna maeneo mengi ambayo wangeweza kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ; they give one the impression that the management is not cost conscious!
Kuna mtu kaniambia mfanyakazi wa chini kabisa crdb anavuta salary ya 1.2m Tena huyo ni mpya aliyeanza kazi, kwahiyo mi naona waachwe tu watumie hela maana wanajali wafanyakazi na wanahisa
 
Nakumbuka mwaka 2015 hisa za CRDB zilikuwa zikiuzwa 410, Magufuli alipoingia zikashuka kwa kasi ya 4G

Samia alipoingia naona zimepanda ghafla tena hadi 430 kutoka 150 in less tha 2 years, ongezeko la 200%

Tukisema yule mtu aliharibu uchumi watu wanatukana
Kama walikuwa wanatumia fedha za serikali kufanyia biashara bila serikali kufaidika, Leo akitokea mtu kubadilisha Hilo tatizo liko wapi!?
 
Kama walikuwa wanatumia fedha za serikali kufanyia biashara bila serikali kufaidika, Leo akitokea mtu kubadilisha Hilo tatizo liko wapi!?
Hisa zinapanda na kushuka kutokana na uwekezaji kupanda au kupungua....... Uwekezaji ulipungua sana nchini kipindi cha Magufuli
 
Jana kulikuwa na mkutano wa wanahisa wa CRDB kule Arusha na katika agenda ya gawio kwa wanahisa waliazimia kuwa kila hisa moja watatoa gawio la Tshs.36. Binafsi kama mwanahisa sijaridhika na gawio la Tshs.36 kwa hisa mpaka nipate majibu kwa yafuatayo:-

(1) Ni vigezo gani mliotumia kufikia kiasi hicho cha Tshs.36 kwa hisa?.
(2) Mbona Benki kama NMB ambayo kwa uwezo hazitofatiani wanatoa gawio zaidi ya Tshs.100 kwa hisa?.

Wajue kuwa kama mwanahisa kwa kweli gawio wanayotoa wanapunja sana wanahisa huku Wakurugenzi na Viongozi wakuu wa Benki wakilipwa marupurupu na fedha nyingi.
By the way, uwekezaji kwenye hisa unahitaji MTAJI mrefu na maarifa ya kutosha. Uwe na pesa ambayo ni stress free, hauiwazii kabisa ikupe faida kubwa, unless uwe ume-stake pesa ndefu.


Aliyeweka million 5 hawezi akawa sawa na yule aliyeweka million 600 in terms of annual dividends.

Tsh 36 Kama dividend yako annually times your number of shares, inaleta ROI ndogo sana kwa wenye MITAJI midogo.

N:B Never buy shares for the sake of buying, hasa ukiwa na pesa kidogo, that's actually a game of numbers, utakuwa unaona pesa yako haileti kile unachokitarajia siku zote.
 
Back
Top Bottom