Gaza: Makombora ya Israel yashambulia kituo cha mpakani upanda wa Misri

Gaza: Makombora ya Israel yashambulia kituo cha mpakani upanda wa Misri

MTZ 255Dar

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2018
Posts
1,149
Reaction score
3,963
Jeshi la Israel limetoa salamu za Pole baada ya kombora lake kupiga kituo cha mpakani cha RAFAH upande wa Misri. Mara nyingi Israel hushambulia kituo hicho lakini upande wa GAZA. Kituo hicho ndio njia pekee ya kutoka na kuingia GAZA ambacho hakidhibitiwi na Israel.

Hata hivyo, Misri bado haijatoa tamko lolote mpaka sasa. Hayo yanajiri baada ya msafara wa pili wa Malori 18 ya msaada wa kibinadamu yakiingia Gaza kutokea upande wa Misri. Hata hivyo Israel imesema Malori hayo yaliingia bila Israel kujulishwa na hivyo kukiuka Usalama wake. Malori ya Msaada 20 ya kwanza yaliingia Gaza baada ya Marekani kuishawishi Israel ikubali msaada huo kuingia GAZA.


View: https://youtu.be/ZB2SqgnkbP0?si=DkmQokKOD6KUwsZ3
Screenshot_20231022-202529.jpg
 
So,kumbe ni vita ya USA against Palestine siyo?

Sasa hiyo nguvu ambayo mnaisifu nayo Israel kumbe bila kusaidiwa hawawez?

Cha ajabu zaidi wakiona Hezbollah na nchi kama Iran zinaside na Palestine wanakasirika na kulalama wanataka vipi Sasa.
Punguza povu. Mbona wakati hamas wanaanza kumshambulia Israel hamkutoa povu hivi?
 
So,kumbe ni vita ya USA against Palestine siyo?

Sasa hiyo nguvu ambayo mnaisifu nayo Israel kumbe bila kusaidiwa hawawez?

Cha ajabu zaidi wakiona Hezbollah na nchi kama Iran zinaside na Palestine wanakasirika na kulalama wanataka vipi Sasa.
Hakuna vita inayopiganwa bila kuwa na nchi nyingine washirika.

Hata WW1 $ WW2 kulikuwa na muungano wa mataifa kadhaa kila upande au Vita ya Uganda na Tanzania kulikuwa na mataifa kama Libya na Palestina walikuwa msitari wa mbele kuipiga Tanzania

Hata leo hii Russia ana washirika wasio waRusi wanaomsaidia kuipiga Ukraine.
 
Lakini US si alisema self defence ni halali (jino kwa jino) au ina-apply kwa baadhi ila sio kwa wengine kama Palestina na hii leo Misri.
Hakuna uhuru usio na mipaka, hata hiyo kauli ina mipaka kwa baadhi ya nchi
 
Duuuuh ila Israel mbabe Sana . Yaani yeye ndo anaruhusu Lori Gani lipite na lipi lisipite 😂😂😂
 
Mipaka au double standard.
Ndo ukweli huo, duniani hakuna usawa wala haki sawa.

Hata hapa Africa kuna double standard dhidi ya watawala na watawaliwa, mfano mtawala akiiba bilioni moja na mtawaliwa akaiba kuku kwa jirani, huyo mtawaliwa anaweza poteza uhai au akafungwa jera wakati mtawala ataendelea kutamba mtaani bila kuguswa.
 
Back
Top Bottom