Gazeti la Mawio lafungiwa kwa miezi 24 kwa kosa la kuwahusisha Mkapa na Kikwete sakata la madini

Gazeti la Mawio lafungiwa kwa miezi 24 kwa kosa la kuwahusisha Mkapa na Kikwete sakata la madini

Point,

ngojea waende mahakamani.
Pia ni aibu kwa serikali hii kwa kuwalinda waharifu wa uchumi kwa kuangalia kinga ya wastafu (marais), hii inaonesha haya yanayofanywa na rais ni maigizo kwani wahusika wanajulikana lakini rais hataki waguswe kwa kuwa wanatoka nyumba moja ccm.

Kama kweli rais anania ya kweli, kinga ya kutoshtakiwa wastafu ifutwe ili ile kauli ya "all people are equal before the law " iwe ni ya kweli na siyo selective kwa wapinzani na maskini
Yaani hata hizo kesi za akina Chenge zikifika mahakani tu mimi nitashangaa akina BM na JK wataponaje. Maana haiwezekani Mawaziri au wanasheria walikuwa wanafanya kazi bila baraka au maelekezo kutoka juu.

Nimeshangaa sana kuona JPM akiongea kwa hasira kwa hao jamaa kuzungumziwa kwenye mikataba.
 
Hapa ndipo serikali inapokosea. Sababu iliyotumika kulifungia hili gazeti ni dhaifu mno.
You are quite right! Kuna wakati serikali inajijengea chuki bila kujua. Hii sababu, hata kama ni AGIZO kutoka JUU, ni dhaifu mno na hukumu imetolewa wakati mbaya sana! Wakati huu ambapo watu wanaanza kuona kwa mapana zaidi athari za kuwapa kinga marais, kulifungia gazeti kwa habari ambayo kimsingi imeanzishwa na serikali yenyewe, ni kosa kubwa la kiufundi. Kuna taarifa inazunguka mtandaoni kwamba Chenge amedai kumkamata wanaweza lakini kumfunga hawawezi kwa sababu alichokifanya ni sawa na alichokifanya Magufuli wakati wa zoezi la kuuza nyumba!-(kutekeleza matakwa ya Rais/Baraza la mawaziri). Sasa katika mazingira haya kufungia gazeti kwa sababu tu ya kuwagusa marais wastaafu ni kutengeneza mgogoro mwingine na jamii unnecessary!
 
hahahah! hapo ndo uone mzee wa makanika Ana nia yeyote ya kupigania huo mchanga zaidi ya self interest apate nae mgao wake
 
jamaa anajua naye akistaafu watu wataamsha dude Kama pesa za kununua bombardier, michango ya kagera n.k
 
Habari za hivi punde ni kwamba, Gazeti la Mawio limefunguwa kwa miezi 24 kutokana na kosa la kuwahusisha Mkapa na Kikwete kwenye mikataba ya madini
View attachment 524471
Mngejua historia ya Mawio na bwana mkubwa tangu alipopitishwa kuwa mgombea msingeshangazwa na hiki kilichotokea! Kuna makala moja ya hatari Mawio walichapisha ilimchambua sana bwana mkubwa, na nina uhakika waliosoma makala ile na kuitafakari kisha wakaielewa, hawakumpa kura!
 
Mwakyembe ana mihemko ya kitoto sana
ameona gazeti limegonga ikulu kabisa bila chenga,kwa kujipendekeza akaona alipige ban 24months ili kabwana mkubwa aone anafanya kazi. hili nalo ni kwa sababu ya stress and depression
 
Naona mwakiembe anajaribu kuutenganisha muwa na sukari.
AMEKOSEA.
 
Sijui nitalipata vp hilo gazeti.Please km umeshalisoma au kwa namna yeyote ile una copy tafadhar naomba tuwasiliane.
 
ila hao wazee si ndio ma sterling wakubwa wa izo issue inakuaje tunapigana biti kusema waarifu
 
Back
Top Bottom