Gazeti la Mawio lafungiwa kwa miezi 24 kwa kosa la kuwahusisha Mkapa na Kikwete sakata la madini

Gazeti la Mawio lafungiwa kwa miezi 24 kwa kosa la kuwahusisha Mkapa na Kikwete sakata la madini

[emoji256]

Wako wa kunikamata ila wakunifunga Hakuna.

Nanukuu :
Nilitia sahihi kweli kama ripoti inavyodai ila kwa maagizo ya boss wangu sasa tatizo liko wapi kwangu?

Aliyetuagiza sisi kutia sahihi ndiye boss huyo huyo aliyemwagiza yeye kuuza nyumba za umma na kama ni kesi zinafanana.

Am not a stupid to sign agreement without a security.

✍✍✍

Shikamoo Mzee Chenge

[emoji115][emoji115][emoji115][emoji120][emoji115][emoji115][emoji115]
Hahahahaha shikamoo tena mzee Chenge, nacheka na vitu havi chekeshi ila ndio hivyo tena
 
Ila KI-UKWELI, Pamoja na kwamba Rais kazuia kuwananga hawa marais wastaafu, ila walikuwa na kesi ya kujibu hapa, ikiwa kinga ingeondolewa, ila na wao wana damu, moyo, nafsi nk. machozi ya watanzania yanawalilia ndani ya mioyo yao, pengine kwa sasa tungekuwa tunakusanya mapato ya Trilioni 2 kwa mwezi, ila kwa Ulofa wao wakakubali kuweka ubongo wao pembeni na kuazima ubongo wa wazungu, baada ya kustaafu ndio ubongo wao umerudi na kuanza kujutia kuwa tulifanya makosa, hata JK. atasema kuwa nilisaini kwa maelekezo ya Mkapa.
Eeebwa so mzigo wote unamwangukia Mkapa.
 
Mwakyembe kajipendekeza hapo, ilitakiwa onyo kali tu..
 
mawio wataenda mahakamani na wataigaragaza ccm vibaya,kumbukeni gazeti hili lilifungiwa mahakama ikalifungua na wanaidai serikali mabilion

Jamuhuri hii haijawahi kufungua kesi za MIHEMKO Kama hizi na WAKABAKI SALAMA, ifike Wakati kesi za MIHEMKO Kama hizi zikikosa kumtia mtu hatiani, gharama za kesi ziwe za mifukoni mwao LABDA TUTAHESHIMIANA
 
Mwakyembe ulikulupuka kama kulinda chakula umejitahidi je! umewaza kesho ukistafu utakua mlinzi kwann
 
Halafu wenyewe mtindio wa ubongo wanatuhimiza tushikamane na rais eti anachukua hatua za kizalendo kulejesha Rasilimali zetu,sasa kama hataki hata tuwataje viongozi waliokuwepo madarakani wakati mikataba hii ya kinyonyaji inasainiwa kile kinachoitwa uzalendo kiko wapi?
Huyu ni msanii kuliko Jakaya
 
Kwa hiyo tubaki na Uhuru,mzalendo na habari Leo? Hata mkitoa na posho kwa wasomaji " sinunui,sisomi"
 
Magufuli kuna kitu anakosea.
Anafanya jambo zuri lakini ndani yake anaweka doa ambalo linachafua lengo lake na kubaki kudharauliwa.

Mfano zoezi la vyeti feki lilikuwa la maana ila lilialibika mwishoni kwa kuwabagua wanasiasa.

Sawa na hili la mchanga kafanya juhudi kubwa ila kaja kuharibu mwishoni

Hakuna mtanzania atakayeelewa kuwa matatizo ya madini kuwa maraisi waliopita hawahusiki kwani wao ndio waliokuwa wasimamizi wakuu.

Nadhani anavitisha vyombo vya habari kuwa hawanahuru wa kuandika mambo ya ukweli but kazi yao iwe mapambio tu.

Magu huweleweki unamalengo yapi
Huweleweki kuwa ni mzalendo wa kweli au ni mnafiki
Kibaya zaidi magufuli ameshajua utamu wa hiki kipendele cha kutokushitaki rais akiwa madarakani. Atakitumia ipasavyo!!
Hapo tayari ameshawalazimisha wanasheria wasaini mikataba ya bormberdier na wala hatapeleka bungeni ijadiliwe. Ameshawalazimisha tayari wanasheria wasaini mkataba wa ujenzi wa chato international airport na hawezi kupeleka sheria husika ipitiwe bungeni na akili kubwa za upinzani.....
 
Mwakyembe kila siku anawaza nitoke vipi...nilitegemea angewapa the right to be heard.hakufanya hivo. Mawio wakienda high court wanaibuka kidedea. Huyu Mzee mwakyembe kachoka apunzishwe uwaziri, sijui taaluma yake ya sheria anaitumiaje,,, nahisi rais atatengua fasta uamuzi huuu wa kileyman...otherwise aliowachagua wanampotosha au wa nafanya matukio kumridhisha,
 
Yaani hata hizo kesi za akina Chenge zikifika mahakani tu mimi nitashangaa akina BM na JK wataponaje. Maana haiwezekani Mawaziri au wanasheria walikuwa wanafanya kazi bila baraka au maelekezo kutoka juu.

Nimeshangaa sana kuona JPM akiongea kwa hasira kwa hao jamaa kuzungumziwa kwenye mikataba.
Kibaya zaidi magufuli ameshajua utamu wa hiki kipendele cha kutokushitaki rais akiwa madarakani. Atakitumia ipasavyo!!
Hapo tayari ameshawalazimisha wanasheria wasaini mikataba ya bormberdier na wala hatapeleka bungeni ijadiliwe. Ameshawalazimisha tayari wanasheria wasaini mkataba wa ujenzi wa chato international airport na hawezi kupeleka sheria husika ipitiwe bungeni na akili kubwa za upinzani.....
 
Back
Top Bottom