Gazeti la MwanaHALISI lafungiwa kwa miaka miwili, wahukumiwa kwa kuandika habari za uzushi kuhusu Mwakyembe na Makinikia

Gazeti la MwanaHALISI lafungiwa kwa miaka miwili, wahukumiwa kwa kuandika habari za uzushi kuhusu Mwakyembe na Makinikia

Kwani hao waliona hakuna weledi wa uandishi wana weledi gani? Kila siku wanashindwa mahakamani. Watayarishe tu hela za kuwapa.
 
Mbona kama vile anarembua ' mimacho ' yake wakati anazungumza hapo? Ni macho yangu tu ' yamekengeuka ' au na wengine mmeliona hilo?
fuata content mkuu mambo ya macho au makalio ni maumbile ya binadam kutoka kwa muumba kazi yake haina makosa
 
Ushauri kwa wamiliki wa Mwanahalisi; Anzisheni gazeti jingine na mlisajili kabisa kwa sababu katika maelezo hayo ya Serikali hamjazuiwa wamiliki kuanzisha gazeti jingine kwa taratibu zile zile. Mnaweza kuliita Mwanajamii.
 
Hivi ni nani mwenye wajibu wakulalmika then gazeti au chombo cha habari kinafungiwa?

manaa sitaki kuamini TBC na UHURU bado vipi hewani nasijawahi kusikia hata ONYO!
 
Mwanahalisi limepoteza credibility.
Ingawaa mpaka hapo sijaona sababu ya kulifungia.
 
WanatakA kutuamisha mjadala wa lisu, hatuliach lkapta iv iv ng'o, lazma unyama huu malpo yapatkane apa apa mbinguni maesabu
 
weledi kwa waandishi wa habari hapa nchini ni jambo la muhimu sana kuzingatiwa. magazeti mengi yamekua yakiandika habari mbali mbali zisizo na vyanzo vya kueleweka au za kuzusha tu kwa minajili ya kuuza kopi nyingi, lakini wanasahau kwamba wanao wajibu muhimu sana wa kuwapa wananchi taarifa sahihi.
Weledi wanao waandishi was Uhuru
 


Msemaji wa serikali:
Mfano tarehe 30 Januari lilichapisha habari yenye kichwa cha habari 'Ufisadi ndani ya ofisi ya JPM' ilhali ndani linazungumzia ufisadi ndani ya shirika la elimu Kibaha, ni kiwango cha juu sana cha sensetionalism. Tuliwaita wakaona udhaifu wao na kuomba Radhi na tukawasamehe.

Miezi miwili baadae April 27 wakaja na habari kubwa Mwakyembe: Maisha yangu yako hatarani. Hii stori ilikuwa ya kutunga, Mwakyembe hakuzungumza popote na mhariri wa Mwanahalisi wala mwandishi yoyote, wakaomba radhi kwenye gazeti lao la Mei kwa mheshimiwa Mwakyembe kwa kuomba Radhi, wakaahidi kwenye gazeti kuchukua hatua za kinidhani kwa mhandishi aliezusha, hatua hatujazisikia hadi leo na bado wameendelea na uandishi huo.

September 4 walikuwa na habari nyingine kubwa 'Makinikia yakwama'. Ni mfano mwingine wa habari ya kutunga, tukawapa muda wasahihishe lakini wakakataa kwa maana hawaoni kosa kisheria. Msingi wa kwanza kwenye uandishi wa habari ni ukweli, kamati ya makinikia imekwama wapi na lini, hata ukisoma Miga ina msingi wa confidentiality, sasa katikati ya mazungumzo gazeti kuibuka na kusema mazungumzo yamekwama.
========

View attachment 591506
View attachment 591504

Wamesahau moja. Gazeti la juzi lilikuwa na screaming headline ikisema KIKWETE ATOA MAZITO KUHUSU TUNDU LISSU, huku kukiwa na picha ya Rais Kikwete pembeni na trademark smile yake. Ukienda ndani ukurasa wa 5 kumbe ni maneno aliyosema Ridhwani Kikwete bungeni mwezi uliopita. Alisema tu kwamba serkali iwadhibiti wauaji wa Kibiti na IMMMA na wabunge.
 
Kama liliongopea kuhusu Mzee wetu Mh.Lowassa kwa hili sishangai
 
WanatakA kutuamisha mjadala wa lisu, hatuliach lkapta iv iv ng'o, lazma unyama huu malpo yapatkane apa apa mbinguni maesabu


Hii misemo imeanza kuota kutu sasa
 
Hii Nguvu itumike kujenga viwanda na kuwabaini watu wasiojulikana.
 
ccm wote wapumbavu nyakati zote ila Hii ni serikali ya kipumbavu kuwahi kutokea TZ
 
wapuuzi mko wengi,walilifungia gazeti la mseto kwa habari iliyomhusu ngonyani lakini mwisho wa siku ukweli umejulikana na ngonyani kajiuzulu kwa habari ile ile iliyosababisha gazeti kufungiwa,
ccm ni mbwa...eti ni watetezi wa raslimali hao mawakala wa mabepari na mafisadi wote
 
Back
Top Bottom