Gazeti la MwanaHALISI lafungiwa kwa miaka miwili, wahukumiwa kwa kuandika habari za uzushi kuhusu Mwakyembe na Makinikia

Gazeti la MwanaHALISI lafungiwa kwa miaka miwili, wahukumiwa kwa kuandika habari za uzushi kuhusu Mwakyembe na Makinikia

Msemaji wa serikali:
Mfano tarehe 30 Januari lilichapisha habari yenye kichwa cha habari 'Ufisadi ndani ya ofisi ya JPM' ilhali ndani linazungumzia ufisadi ndani ya shirika la elimu Kibaha, ni kiwango cha juu sana cha sensetionalism. Tuliwaita wakaona udhaifu wao na kuomba Radhi na tukawasamehe.

Miezi miwili baadae April 27 wakaja na habari kubwa Mwakyembe: Maisha yangu yako hatarani. Hii stori ilikuwa ya kutunga, Mwakyembe hakuzungumza popote na mhariri wa Mwanahalisi wala mwandishi yoyote, wakaomba radhi kwenye gazeti lao la Mei kwa mheshimiwa Mwakyembe kwa kuomba Radhi, wakaahidi kwenye gazeti kuchukua hatua za kinidhani kwa mhandishi aliezusha, hatua hatujazisikia hadi leo na bado wameendelea na uandishi huo.

September 4 walikuwa na habari nyingine kubwa 'Makinikia yakwama'. Ni mfano mwingine wa habari ya kutunga, tukawapa muda wasahihishe lakini wakakataa kwa maana hawaoni kosa kisheria. Msingi wa kwanza kwenye uandishi wa habari ni ukweli, kamati ya makinikia imekwama wapi na lini, hata ukisoma Miga ina msingi wa confidentiality, sasa katikati ya mazungumzo gazeti kuibuka na kusema mazungumzo yamekwama.
========

View attachment 591506
View attachment 591504

Headline inayostahili ni kwamba Mwanahalisi limefungiwa kwa kuchapisha makala yenye hoja za Lissu zinazolinganisha uzalendo wake na wa mwenyekiti wa CCM!
 
Sijawahi na wala Sihitaji kwani kula kwa kutumia ujinga wa watu ni tendo baya sana. Mimi pia siyo mpenzi wa udaku hivyo vijarida kama hivi vya waganga njaa havichukui muda wangu.
Mbona hoja zako huwa zinaku reflect kama msomaji wa Wembe na Sani?
 
kwa hiyo unafanyaje sasa mkuu? maana ushanichagulia upande

hivi unaweza ku dispute sababu hizo walizozitoa? mbona mwananchi haikumbani na hiyo kadhia? mbona gazeti kabisa la chadema "Tanzania Daima" haikumbani na hii kadhia

anayeonekana mjinga ni nani hapa?
Rudi kwenye hoja yako. Hata hivyo, ili nikusaidie staili za uhariri za Mwanahalisi na Mwananchi au Tanzania Daima ni tofauti. Kama umeisoma taarifa ya Dk Abbas ungeona haraka kwamba sababu ya kufungia Mwanahalisi ni moja tu-kuchapisha makala inayoonyesha kwamba Lissu ni mzalendo kuliko mkuu, period!
 
Yupo wapi Mhandisi Edwin Ngonyani hivi leo? Mwanahalisi walifungiwa kwa kureport mapema ishu yake ya madini.. Leo hii ametumbuliwa ukweli umejulikana. hata huyo mkuu kuna siku atajikuta kwenye angle nzuri..
 
Haswaa!!! Ila ingekuwa ya kizushi na chonganishi na baadae wakihojiwa wangeomba radhi.
Kama ilivyokuwa ya kizushi ile ya Naibu waziri Ngonyani ambayo gazeti la Mseto lilipoandika likafungiwa, lakini Magufuli alipomfuta kazi kwa sababu zile zile ambazo ziliandikwa na Mseto kama kawaida yenu mkampigia makofi Magufuli. Ingekuwa ya kizushi kama vile tu ya Ulimboka. Acheni woga jipangeni kuwa mnajibu hoja!
 
Lakini mara zote mahakama imekuwa ikithibitisha kuwa sio wazushi. Na mlivyo watu wa ajabu hata Mawio walipoandika kuhusu aliyekuwa naibu waziri Ngonyani Mawio lilifungiwa mkashangilia, lakini jambo la ajabu hata juzi waziri huyo huyo alipotakiwa na Magufuli ajiuzulu baada ya kutajwa na Kamati ya Bunge kwenye madini kwa jambo lile lile lililoandikwa na Mawio likafungiwa, mkashangilia tena. Nchi hii inaangamia kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wa aina yenu!
I like great thinker like you achana na wasiojielewa na ndio maanawanahasira na D.Uchwara wao
 
Limezuia kuanzisha viwanda??
Haituhusu.. kama limekiuka maadili ya uandishi lifungiwe milele. Hata hivyo mmelibeba sana kwa makosa mengi ambayo wamekuwa wakifanya. Mna huruma mmnoo..lingefungiwa maisha. Tunamtaka Kub.ene.a arudi darasani amalizie shule yake ya msingi kama sikosei.
 
Kama ilivyokuwa ya kizushi ile ya Naibu waziri Ngonyani ambayo gazeti la Mseto lilipoandika likafungiwa, lakini Magufuli alipomfuta kazi kwa sababu zile zile ambazo ziliandikwa na Mseto kama kawaida yenu mkampigia makofi Magufuli. Ingekuwa ya kizushi kama vile tu ya Ulimboka. Acheni woga jipangeni kuwa mnajibu hoja!
Gazet hilohilo liliandika Lowasa hasafishiki...lakini kwa mshangao walimsafisha wemyewee..siasa gani hizi za udanganyif mchana kweupee
 
Mtu aligeuzwa kuwa chekeche pale Dom karibia na nyumba ya sipika sembuse kufungia gazeti.Kazi ndogo sana hiyo katika ujenzi wa viwanda vya chuki.
 
Haituhusu.. kama limekiuka maadili ya uandishi lifungiwe milele. Hata hivyo mmelibeba sana kwa makosa mengi ambayo wamekuwa wakifanya. Mna huruma mmnoo..lingefungiwa maisha. Tunamtaka Kub.ene.a arudi darasani amalizie shule yake ya msingi kama sikosei.
Ndo matatizo ya wivu wa kike.kubenea na gazeti vimekujaje hapa??umaskini wa mawazo ni mbaya sana,huharibu roho na utu wako babel.kuwa wa kiume,pambana na hali yako
 
Subiria huo mwisho mpaka unazeeka
Kuwa na akili ww usikatishe tamaa watu kila kitu kina mwisho ww na si lazima uzeeke kwa maana huijui kesho yako, Hata Nape alikuwa kama ww na yy akawa wakwanza kuonyeshewa mashine hadharani na mpka leo haamini
 
Ukweli kabisa now mwigulu anajuta kuwa waziri wa mambo ya ndani coz anatumika
Muulize makamba January kinachomkuta
 
Kama ilivyokuwa ya kizushi ile ya Naibu waziri Ngonyani ambayo gazeti la Mseto lilipoandika likafungiwa, lakini Magufuli alipomfuta kazi kwa sababu zile zile ambazo ziliandikwa na Mseto kama kawaida yenu mkampigia makofi Magufuli. Ingekuwa ya kizushi kama vile tu ya Ulimboka. Acheni woga jipangeni kuwa mnajibu hoja!
Nilicomment baada ya kuona maelezo na vielelezo vilivyotolewa na Serikali na kuanisha na comment iliyotolewa na mchangia mada. Na hata wewe inaonekana katika hili la Mwanahalisi huna la kulitetea ndio maana umehamishia magoli Mawio. Huwa sicomment nisichokijua kama hilo la Mawio ulilolileta.
 
Kuwa na akili ww usikatishe tamaa watu kila kitu kina mwisho ww na si lazima uzeeke kwa maana huijui kesho yako, Hata Nape alikuwa kama ww na yy akawa wakwanza kuonyeshewa mashine hadharani na mpka leo haamini
Nape unayemsema ana njaa ya uwaziri siku akipewa atatulia kama kitila mkumbo
 
Miaka miwili ?Uhuru wa vyombo vya habari upo Wapi ?Tanzania kama Uturuki.
Uhuru bila uwajibikaji you endup in anarchy (mpatampatae). Hakuna uhuru usio na mipaka; kwa hili, moja ya hiyo mipaka ni kuandika ukweli. Ukiandika uongo lazima uwe tayari kubeba consequences zake.
 
Back
Top Bottom