Gama
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 13,265
- 4,735
Mimi hupenda kusoma magazeti kwa sababu mbalimbali. Katika magazeti ya nyumbani Gazeti la mwananchi halikosikani katika menu yangu pale inapowezekeana
Mada
Leo nimesoma article inayosema "Harufu kali machinjio ya Vingunguti yaleta kilio". Kilichonifanya kuandika humu si harufu wala kilio, ni picha iliyosakinishwa ikiwa na maelezo kuwa mtu anayeonekana akichekeka - anachekecha damu. Hii ndo story iliyonisikitisha kwakuwa ukweli ni kuwa mtu anayeonekana pichani hachekechi damu bali anachekecha Udongo. How pissible is this?, huo udongo unatoka wapi?, nini matumizi ya huo udongo?, je unajua kuwa udongo huu unachangia kuua uchumi wa watu pamoja na kuhatarisha afya ya mamilioni ya watanzania?, Kwanini mwananchi hawakuliona hili?
Huo udongo unatoka wapi: Udongo huu unachimbwa katika eneo lililokuwa dampo pembezoni mwa kingo za mto msimbazi.
Udongo huu unamatumizi gani: Udongo huu huchimbwa, huanikwa ili ukauke kisha unapondwa na kuchekechwa ili kupata udongo usio na vitu vingine. Kisha udongo huu huloweshwa tena na kutengeneza tope, tope hili husambazwa kwenye tent la kuanikia damu iliyochemshwa kisha huchanganywa na damu iliyochemshwa.
Lengo ni nini: Lengo ni kuongeza uzito wa damu na kupata fedha nyingi zaidi, inakadiliwa kuwa mchanganyiko ni 1:2 or 1:3 yani damu kipimo kimoja kwa vipimo vitatu vya udongo;
Hii ina madhara gani:
1. Udongo huu unakiasi kikubwa cha heavy metals, hiki ni kisababishi kikubwa cha magonjwa hasa ya kansa na viungo kama ini na figo, hii inatokana na sababu kuwa kuku akila damu iliyochanganywa na huu uchafu mwili wake hauwezi ku-digest hizi heavy metals hivyo huweza kupasishwa hata kwa mlaji ambaye ni mimi na wewe.
2. Udongo huu una vimelea vingi vya magonjwa kama E.coli, minyoo, na jamii nyingine za salmonela. hivyo, damu hii ikitumika kutengeneza chakula cha mifugo hupasishwa vimelea hivyo kwa mfugo na hivyo kuleta gharama kubbwa ikiwemo ya matumizi ya dawa za tiba kwa kiiasi kikubwa hivyo kupunguza faida ya mfugaji.
GAZETI LA MWANANCHI, NENDENI MFANYE HOMEWORK VIZURI ILI MUOKOE WATANZANIA WANAOANGAMIA KWA KUKOSA TAARIFA