Gazeti la serikali ni nini na linauzwa wapi?

Gazeti la serikali ni nini na linauzwa wapi?

Naomba anayejua maana ya gazeti la serikali ni nini. Naskia skia tu gazeti la serikali lakini sifahamu ni gazeti la HabariLeo au Daily News au ni lipi hilo?Msaada pls.
Temebelea website ya Public Service Management nenda kwenye sub-title ya publication utaona Government gazette, clip hapo utakuta copy za hilo gazeti za kila mwezi mkuu....naamini nitakuwa nimetoa msaada kwako
 
Naomba anayejua maana ya gazeti la serikali ni nini. Naskia skia tu gazeti la serikali lakini sifahamu ni gazeti la HabariLeo au Daily News au ni lipi hilo?Msaada pls.

Ni gazeti rasmi kwa serikali,na matangazo yake,ikiwemo marekebisho ya sheria,tangazo ya sheria mpya na kanuni,miongozo,uthibitisho,pamoja na uteuzi rasmi,kati ya mengineyo!
 
Kichwa chajieleza, kwa muda mrefu nimekuwa nikisikia kuwa kuna gazeti la serikali ambalo hutangaza tenda, sheria mpya nk.hivi likoje na huuzwa wapi?
Huandikwa na kina nani? lini? na wapi?
msaada please.
 
Ni HabariLeo na DailyNews mkuu au Kama nimekosea wajuvi wanakuja
 
Gazeti la TBC taifa

Kama siyo juhudi zako nyerere na Uhuru tungepata wapiii x2
 
Swali ni la msingi sana hili,ingawa muulizaji naye!mmh....Gazeti la serikali ni gazeti maalum linalochapisha matangazo,maamuzi yote ya serikali linapatikana idara ya habari maelezo.
 
Swali ni la msingi sana hili,ingawa muulizaji naye!mmh....Gazeti la serikali ni gazeti maalum linalochapisha matangazo,maamuzi yote ya serikali linapatikana idara ya habari maelezo.
Umejibu vizuri. Watu wanachanganya na hata watawala wanachanganya vyombo vya habari vya umma kama TBC, Daily news, habari leo. Hivi ni vyombo vinavyotakiwa kuweka mbele masalah ya umma habari za umma lakini vyenyewe vimejigeuza kuwa mdomo wa serikali na mda mwingine vimejigeuza kua vya chama cha mapinduzi. Vyombo vya umma vinaendeshwa na kodi zetu. Ukiona wananchi hawaviangalii na wala hawavihesabu km vyombo vya habari ujue kuna tatizo. Tena tatizo kubwa. Mfano jiulize bbc au dw navyo Vina status sawa na TBC. Lakini vinaaminika na vimeweka mbele maslahi ya umma wao. Tuna safari ndefu sana
 
Kichwa chajieleza, kwa muda mrefu nimekuwa nikisikia kuwa kuna gazeti la serikali ambalo hutangaza tenda, sheria mpya nk.hivi likoje na huuzwa wapi?
Huandikwa na kina nani? lini? na wapi?
msaada please.
.
Mkuu, Gazeti la serikali (Government Gazette) ni chapisho linalochapisha habari zote rasmi za serikali (sio hotuba au matamko ya kisiasa). Si gazeti kama magazeti mengine, isipokuwa ni mkusanyiko wa taarifa mbalimbali zinazotakiwa kuufikia umma. Gazeti hili huchapishwa walau mara moja kwa wiki.

Matamko mbalimbali ya kitaifa yanayofanywa na wizara au mawaziri, raisi na viongozi wote wa umma huchapishwa kwenye gazeti hili ili kuyapa matamko haya nguvu ya kisheria. Gazeti hili unaweza kulipata kirahisi katika duka la serikali. Mfano wa gazeti halisi huu hapa chini
 
Attachments

Umejibu vizuri. Watu wanachanganya na hata watawala wanachanganya vyombo vya habari vya umma kama TBC, Daily news, habari leo. Hivi ni vyombo vinavyotakiwa kuweka mbele masalah ya umma habari za umma lakini vyenyewe vimejigeuza kuwa mdomo wa serikali na mda mwingine vimejigeuza kua vya chama cha mapinduzi. Vyombo vya umma vinaendeshwa na kodi zetu. Ukiona wananchi hawaviangalii na wala hawavihesabu km vyombo vya habari ujue kuna tatizo. Tena tatizo kubwa. Mfano jiulize bbc au dw navyo Vina status sawa na TBC. Lakini vinaaminika na vimeweka mbele maslahi ya umma wao. Tuna safari ndefu sana
Hapo umejibu au umelalamika?
 
Linapatikana kwenye maduka ya serikali au kwa mpigachapa ws serikali. Linachapishwa mara moja kwa mwezi.

Ukifika kwenye maduka ya serikali watakupa jibu zaidi
 
Wakuu wasaalam.

Nimekuwa nikisikia kuna gazeti linaitwa "Gazeti la Serikali". Binafsi silifahamu na kwa kweli sijawahi kuliona. naomba kulifahamu gazeti hili kwa mfano je linaandika habari zipi, waandishi wake ni nani? wanaandika habari zipi? je naweza kuwapelekea stori zangu? je linauzwa au ni la bure? Kama linauzwa linauzwa wapi na Je naweza kuweka oda niwe naletewa kwenye kijiwe changu pale tabata?.
 
mkuu hilo duka la serikali linapatikana wapi
Lilikuwepp moja jirani na benjamini mkapa pale posta....sidhani kama linafanya kazi....

Labda ujaribu kiwandani pale chang'ombe (darajani pale jirani na maliasili)
 
Back
Top Bottom