Gazeti la Tanzania daima la leo kanini halijaripoti kikao cha viongozi wa CHADEMA na CCM?

Gazeti la Tanzania daima la leo kanini halijaripoti kikao cha viongozi wa CHADEMA na CCM?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Nimeona kwenye gazeti la Mwananchi la leo limeandika kwamba uongozi wa CHADEMA na CCM walikutana jana kwa saa nne.

Nikatamani niisome Ile habari kwenye gazeti la Tanzania Daima ili niipate kwenye chanzo sahihi.

Cha ajabu sijaiona kabisa hiyo habari. Ndipo nikapata maswali mengi sana. Kwa nini wasiiandike? Waliona haina umuhimu? Waliona ni habari inayowaaibisha?

Ila Kwa maoni yangu naona hiki kikao ni habari kubwa Kwa CCM kuliko Kwa CHADEMA.

Ni kama CCM imewamudu wapinzani wake wote. CHADEMA wanatamani wawe wakubwa sana Kwa kukimbia kikosi kazi, lkn wamejikuta kwenye uwanja kama ule ule wa kikosi kazi.

Kama CHADEMA wako serious na wanataka kujitutumua wanapaswa kugomea Kila kitu alafu warudi kwa wananchi, waweke shinikizo Kwa kiwango ambacho CCM iwatafute.
 
Mageuzi ya nchi ni sehemu ya kila mtu popote anapoishi kuwaachia vyama ni kufikiri Kwa uwezo mdogo
 
Wanasema busara ni kuitikia mwito,japokuwa ukusema hapa nani kamwita mwenzie.
Ukishafika na kusikiliza,ni juu yako kukubali au kukubali kutokubaliana na mazungumzo yenu,baada ya kuyatafakari nakuyachuja kwa kina.
 
Back
Top Bottom