Gazeti la The Citizen lahoji nani aliishauri Serikali kujenga SGR wakati wataalamu wanasema italeta hasara?

Hizi makala huwa haziibuki tu, hii ni propaganda yenye lengo maalum. Hii nchi kuna ujinga tunaulea, kuna mambo tukiruhusu siasa zetu chafu ziingilie tutavuna mabua.
 

Hii makala iko kimkakati kabisa baadae mtakuja kusema kuwa serikali haina hela hahaha mwananchi wanalipwa kuandika makala kama hii na wanalipwa na wenye jukumu la kusimamia mradi huuu
[emoji1787] hahahaha
 
Kila mradi unakuwaga na sunk cost , naona nikikufafanulia zaidi hutakuwa tayari kuelewa kwa sababu uko unaandika ukiwa na upande tayari na unaongea na kivuli pembeni
 
Binafsi niliona halikuwa wazo zuri kwa kuangalia utilization ya reli ya zamani ilikuwa asilimia ngapi? binafsi niliamini tulipaswa kuhakikisha kwanza reli ya zamani ni productive na utilization yake ni maximum na tumeelemewa ndio twende kwenye option B.

Kama tulijenga tu kwa fassion kwa sababu duniani zinajengwa bila technical calculation ni kuchezea tu hela za walipa kodi, watu wetu wanapaswa kuwa na fikra za kazi zaidi.
 
Jamaa lilipenda sifa za kijinga tu na uwezo wa fedha hakuwa nao.
 
Jinga Sana, 🚮 SGR ni mpango wa mda mrefu wa mkapa na sio Magufuli. Yy alikuna kutekeleza,alafu usiwe na chuki ya kike,hata unamchukia Magufuli sio hivyo aisee! Umesahau Kikwete alisaini huu mradi na Wachina watujengee Reli kama Ile ya Kenya iliyojaa ufisadi,na inayotumia diesel, Magufuli akaja kuokoa jahazi,Leo hii mnamsingizia mwenda zake? Laana hii.
 
tusicopy sana modern style of life bila kuangalia stage tuliyopo na nini tunataka wakati huu. Binafsi naamini kwenye uwekezaji wa reli ya zamani iwe productive kwanza maana utilization yake ilikuwa minimum almost zero kwangu, ukiwauliza hawa viongozi watu kwa % ngapi reli ya zamani toka tumeichukua kwa mkoloni imechangia pato letu basi utakutana na vichekecho.

Rail network ya zamani ilipaswa kuwa maintained na kuweka network za kutosha kila mahala linking na major productive cities mpaka kwenye ports zetu, boosting economic activities ambazo zitatumia reli kama kilimo, mining activities kama Coal, graphites nk.

Hatufanyi proper Calculations based on data collection kwenye maamuzi yetu. Kila maamuzi yanapaswa kubase kwenye research na data then watu ndio waamue sio matakwa tu ya mtu akilala na kuamka anaamua.
 
Ninakumbuka ujenzi wa SGR ulipitishwa na kikao cha EAC ndiyo sababu Tanzania na Kenya zilianza pamoja kujenga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…