Hii nchi miaka 60 sasa hata kuendesha mashirika ya maji yanayotumia teknolojia nyepesi sana ili watu wote wapate maji ya bomba bado ni mtihani mzito!
Ngoja nikwambie jambo mkuu 'Yoda'.
Kama hatutafanikiwa kupata viongozi watakaobadilisha mienendo ya waTanzania, toka kwenye hii hali ya maneno maneno mengi, kutojali sana hata panapoharibika; kujifanya ujuaji mwingi, tupo kwenye matatizo makubwa sana.
Sisi hatuna tabia ya kuona uchungu, na kutaka kufanya kama wengine wanavyofanya kwa mafanikio.
Chukulia mashirika yetu yote, kazi ni mzaha mzaha tu na kujisifu kwingi; kelel chungu nzima, lakini matokeo sufuri kabisa, hasara kila mwaka!
Si unasikia kelele tele huko serikalini sasa, kuhusu kuongezwa mishahara? Husikii hata mmoja wa viongozi akizungumzia matokeo (productivity) ya wafanya kazi hao, hakuna!
Ukisikiliza maneno matamu na kujifanya ujuaji; utasikia maneno "sustainable" (najua kuna kiswahili chake, lakini limenitoka), utasikia majivuno na ujuaji wa maana ya neno hilo, lakini nenda kaangalie kinachofanyika, utaona mambo tofauti kabisa!
Nchi itaendelea vipi namna hii?
Vijana wanasoma, wanatoka mashuleni utadhani wamemaliza kila kitu, kilichobaki ni kujigamba kwa digrii zao, lakini hakuna la maana wanalofanya, na wala hawana 'ambition' za kwenda mbele
Nchi yetu sasa hivi inahitaji kiongozi mwenye maono ya kujua ni nini kinatakiwa kufanyika kubadili 'mentality' mbovu kabisa ambayo waTanzania wanayo sasa hivi
Juzi umesikia Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Katibu Mkuu wake wakipiga marufuku uingizaji wa vifaranga toka nje. Lakini wakati wanafanya hivyo, hawa watu hata hawajui ni vifaranga vingapi vinahitajika nchini, na wala hawajui kiasi kinachozalishwa sasa hivi!
Kama siyo maajabu haya tuyaite kitu gani?
Kila mahali unapoangalia, ni uozo mtupu. Nchi itaendelea vipi katika hali ya namna hii.
Hili siyo swala la Ujamaa wala Ubepari. Ni swala la tabia za watu ni mbovu, na hakuna viongozi wanaoweza kuwastua watu wao wabadili hali hiyo.
Acha nisiandike gazeti hapa, lakini ukweli ni kwamba inakatisha tamaa sana.