Gazeti la The Citizen lahoji nani aliishauri Serikali kujenga SGR wakati wataalamu wanasema italeta hasara?

Gazeti la The Citizen lahoji nani aliishauri Serikali kujenga SGR wakati wataalamu wanasema italeta hasara?

Mwalimu Lwaitama atahadharisha kuhusudu kuabudu maendeleo ya vitu bila kufikiri kwanza

Mwalimu Azavery Lwaitama aonya kutwekwa na dhana ya maendeleo ya vitu inaweza kutufanya kutofikiri kwa kina na kupelekea hasara ndefu endelevu kwa uchumi wa taifa na raia wake
 
Hii nchi miaka 60 sasa hata kuendesha mashirika ya maji yanayotumia teknolojia nyepesi sana ili watu wote wapate maji ya bomba bado ni mtihani mzito!
Ngoja nikwambie jambo mkuu 'Yoda'.

Kama hatutafanikiwa kupata viongozi watakaobadilisha mienendo ya waTanzania, toka kwenye hii hali ya maneno maneno mengi, kutojali sana hata panapoharibika; kujifanya ujuaji mwingi, tupo kwenye matatizo makubwa sana.

Sisi hatuna tabia ya kuona uchungu, na kutaka kufanya kama wengine wanavyofanya kwa mafanikio.

Chukulia mashirika yetu yote, kazi ni mzaha mzaha tu na kujisifu kwingi; kelel chungu nzima, lakini matokeo sufuri kabisa, hasara kila mwaka!

Si unasikia kelele tele huko serikalini sasa, kuhusu kuongezwa mishahara? Husikii hata mmoja wa viongozi akizungumzia matokeo (productivity) ya wafanya kazi hao, hakuna!

Ukisikiliza maneno matamu na kujifanya ujuaji; utasikia maneno "sustainable" (najua kuna kiswahili chake, lakini limenitoka), utasikia majivuno na ujuaji wa maana ya neno hilo, lakini nenda kaangalie kinachofanyika, utaona mambo tofauti kabisa!

Nchi itaendelea vipi namna hii?

Vijana wanasoma, wanatoka mashuleni utadhani wamemaliza kila kitu, kilichobaki ni kujigamba kwa digrii zao, lakini hakuna la maana wanalofanya, na wala hawana 'ambition' za kwenda mbele

Nchi yetu sasa hivi inahitaji kiongozi mwenye maono ya kujua ni nini kinatakiwa kufanyika kubadili 'mentality' mbovu kabisa ambayo waTanzania wanayo sasa hivi

Juzi umesikia Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Katibu Mkuu wake wakipiga marufuku uingizaji wa vifaranga toka nje. Lakini wakati wanafanya hivyo, hawa watu hata hawajui ni vifaranga vingapi vinahitajika nchini, na wala hawajui kiasi kinachozalishwa sasa hivi!
Kama siyo maajabu haya tuyaite kitu gani?

Kila mahali unapoangalia, ni uozo mtupu. Nchi itaendelea vipi katika hali ya namna hii.

Hili siyo swala la Ujamaa wala Ubepari. Ni swala la tabia za watu ni mbovu, na hakuna viongozi wanaoweza kuwastua watu wao wabadili hali hiyo.

Acha nisiandike gazeti hapa, lakini ukweli ni kwamba inakatisha tamaa sana.
 
Okay nimekusikia, unapokwenda kukopa hala benk ya ndani Bank watakueleza hebu leta write-up yako juu ya huuu maradi na wanachoangalia ni viability(investment, Technology, soko, returns etc.) ndani yake lazima waangalie fedha hizi wanazokupa utazirudishaje kwenye mradi huu. Kwa Inward looking like you hutapata mkopo hata ufanyeje. SGR haiwezi ku-break even kwa kutegemea soko la ndani hayo mengine ni siasa tu sio uchumi. Na kwa mtazomo huu hata kwa ndege serikali itaendelea kulibeba kwa fedha za walipakodi hadi ndege hizo hadi zichakae. Hata hao ATC wameshaliona ndio unaona wanaanza kwenda India na China sio kutosheleza ruote za Songea na Katavi laa hasha. Think outside the box man.
Tunajenga kwa Kodi zetu, ikibidi tunakopa na kulipa kwa Kodi zetu, mfano serikali imekopa na kujenga Barabara ya lami tabora hadi Mpanda, unategemea huo mkopo utalipwaje?
 
Mkuu inaonekana unachuki binafsi na mwenda zake. Lakini anyway 7 billion wasted in royal tour.

#ROYAL TOUR ikichunguzwa ni hasara ya karne.
 
Ukiamua kujenga nyumba saiv na uje ujenge 2030 hakuna usawa, kuna mfumuko wa bei kila kukicha, reli inajengwa kama hutaki kaa chini ulie.
Acha fujo dogo.. pesa za nchi siyo kama zako unaenda kutoa kwa wakala unajenga banda huko goba.. mradi unaojengwa kwa pesa ya nchi ni lazima ufanyiwe upembuzi yakinifu ili kuona manufaa na hasara zake.. kama hasara ni kubwa kuliko manufaa, huo mradi unafia hapo hapo..
Jiwe aliibuka na sgr kama alivyoibuka na chato bila feasibility study iliyonyooka.. ndo hivyo tunaenda kushuhudia white elephant ndani ya muda si mrefu..
Hawa wahujumu lazima ifike mahali wawe wananyongwa hadharani
 
Ujenzi wa reli kwa kiwango cha SGR ni mkakati mpana wa kuiunganisha Afrika nzima kwa njia ya reli. Eneo letu la Afrika mashariki pia linatekeleza mpango huo na Kenya Tayari waliishaanza, Sisi tunafuata. Afrika Magharibi wako kwenye matayarisho wakati Egypt wameisha anza pia.

Tanzania kuzungukwa na nchi nane kuacha kujenga sasa reli mpya yenye uwezo mkubwa wa kubeba mzigo mzito, ingekuja kutugharimu sana baadaye.

Mpango wa kujenga reli ya SGR, haukuasisiwa na Magufuli bali aliukuta na kuuanzisha kwa kasi ya ajabu. Ni miundombinu ya kimkakati itakayochochea uchumi wetu siku za usoni ....Kama itakamilika!.
Sgr kuhitajika kwa vile tunapakana na chi 8 siyo hoja ya msingi.. hoja ni je, mzigo upo?

Ukweli ni kwamba mzigo haupo, uliopo ni 28% ya kiwango cha chini kuendesha sgr kwa faida. Sijui ambacho hujaelewa nini kwenye hiyo makala? Au kidhungu 🙌
Kwa ufupi, sgr kwa mujibu wa bwn Makakala haina mashiko kwa sababu haitaweza kujiendesha bila ruzuku ya serikali.. tazama serikali ilivyochoka.. inawaongezea watumishi wake sh elfu nane baada ya miaka 7.. wakati gharama za maisha zimepanda mara mbili ndani ya muda huo

Ndo utajua hujui
 
Hao researchers ni manenge na mandawa .kwa hiyo mwisho 2030 ndo mwisho wa Dunia. Siku workd bank watakaposhangilia kuwa Africa inafanya vizuri ujue ndo utakuwa mwisho wa dunia
 
Reli wakati wa mkoloni ilikuwa bize sana na ndiyo iliyotumika kuimaliza Tanganyika na Africa kwa kusafirisha malighafi ya kila aina. Wakati wa mkoloni kwamfano reli ya Dar-Arusha ilikuwa bize ikibeba kahawa leo hii reli hii imekufa.
Iiikuwa bize kwa sababu wakoloni walikuwa wanafanya kazi. Mashamba yote ya kahawa arusha na moshi yalikuwa ya kwao.. ngano kule hanang ilikuwa ya kwao, katani yote kuanzia pangani hadi same ilikuwa ya kwao. Baada ya wivu wa kishamba uliopelekea kutaifishwa kwa hizo engine za uchumi, haikuchukuwa muda mrefu reli ya Arusha-Tanga-Dar kufa..
Tatizo ni mzigo.. treni haisafirishi hewa..

Ndo kitakachoikuta sgr ya mwendazake
 
Hao researchers ni manenge na mandawa .kwa hiyo mwisho 2030 ndo mwisho wa Dunia. Siku workd bank watakaposhangilia kuwa Africa inafanya vizuri ujue ndo utakuwa mwisho wa dunia
Tatizo huenda hilo yai la bwn Makakala limekupita kushoto ndo maana unaandika ambayo hata wewe huelewi.. kasome upya
 
A 2013 World Bank report observed that an SGR project requires a volume of 55 million tonnes to be viable, while EAC railways are estimated to achieve only 14.4 million tonnes in total by 2030.
Hii reference ya zamani Kuna mambo mengi yamebadirika!
 
Hata hii miradi ya barabara za lami wakitukokotolea hao wataalamu ni kwamba hazijawahi kuleta faida hiyo ya kwenye makaratasi sawasawa na ndege tu.
 
Sgr kuhitajika kwa vile tunapakana na chi 8 siyo hoja ya msingi.. hoja ni je, mzigo upo?

Ukweli ni kwamba mzigo haupo, uliopo ni 28% ya kiwango cha chini kuendesha sgr kwa faida. Sijui ambacho hujaelewa nini kwenye hiyo makala? Au kidhungu 🙌
Kwa ufupi, sgr kwa mujibu wa bwn Makakala haina mashiko kwa sababu haitaweza kujiendesha bila ruzuku ya serikali.. tazama serikali ilivyochoka.. inawaongezea watumishi wake sh elfu nane baada ya miaka 7.. wakati gharama za maisha zimepanda mara mbili ndani ya muda huo

Ndo utajua hujui
Naona umejikita kwenye malumbano ya kisiasa. Mzigo usingekuwepo, Rwanda wasingehangaika kujenga bandari kavu Isaka wala wasingekuwa na mpango wa kujenga reli ya SGR kuanzia Isaka-Kigali hadi Goma.

Congo DRC na Burundi, kama wasingekuwa na mzigo wasingehangaika kujenga bandari kavu Kwala, wala wasingejenga reli ya SGR pia, kuanzia Uvinza -Msongati na kisha Uvira-upande wa DRC

Mzigo unaoshuka bandari ya Dar es salaam na Mombasa kuelekea nchi za maziwa makuu ni mkubwa, tatizo liko kwenye miundombinu na zaidi sana ufanisi wa mamlaka za bandali na reli na hasa mind set ya watendaji.

Angali meli siku hizi zinashusha magari 3000 na 80% yanatumia barabara kwenda Burundi DRC na Rwanda walioagiza mzigo. Vipi kuhusu mzigo wa shaba kutoka jimbo la Katanga DRC, unafahamu kuwa ulikuwa unabebwa na TRC hadi bandarini Dar es salaam ?
 
Naona umejikita kwenye malumbano ya kisiasa. Mzigo usingekuwepo, Rwanda wasingehangaika kujenga bandari kavu Isaka wala wasingekuwa na mpango wa kujenga reli ya SGR kuanzia Isaka-Kigali hadi Goma.

Congo DRC na Burundi, kama wasingekuwa na mzigo wasingengaika kujenga bandari kavu Kwala, wala wasingejenga reli ya SGR pia, kuanzia Uvinza -Msongati na kisha Uvira-upande wa DRC

Mzigo unaoshuka bandari ya Dar es salaam na Mombasa kuelekea nchi za maziwa makuu ni mkubwa, tatizo liko kwenye miundombinu na zaidi sana ufanisi wa mamlaka za bandali na reli na hasa mind set ya watendaji.

Angali meli siku hizi zinashusha magari 3000 na 80% yanatumia barabara kwenda Burundi DRC na Rwanda walioagiza mzigo. Vipi kuhusu mzigo wa shaba kutoka jimbo la Katanga DRC, unafahamu kuwa ulikuwa unabebwa na TRC hadi bandarini Dar es salaam ?
Sawa mkuu.. siasa aside..
Hizi nchi unazozizungumzia hazizalishi mali yoyote ya kiviwanda, kiasi kwamba mizigo yake itashindwa kutoka au kufika bandarini.. swala kwamba wanataka kujenga ni sawa tu, ila mahesabu hayako upande wao. Kama kweli mzigo upo.. basi wasingeenda Washington au Beijing kutembeza mabakuli kuomba pesa za miradi..
 
Mkuu kutembeza mabakuli ulaya ni hulka mbaya tuliyonayo waafrika,hasa viongozi wa kisiasa tuliowapa nyadhifa, naamini ni athali za kutawaliwa kiakili na kuacha wanaoitwa washirika wa maendeleo wakivuna mali. Maliasili iliyoko Congo kwa mfano inatumika Dunia nzima ni adimu. Njia ya kulifikia soko la Dunia ni hizi bandari mbili za Mombasa na Dar es salaam. Kuwa na viwanda ili kuchakata malighafi asilia ni hatua ya pili inayotanguliwa na miundombinu imara hasa ya reli.
 
Tunajenga kwa Kodi zetu, ikibidi tunakopa na kulipa kwa Kodi zetu, mfano serikali imekopa na kujenga Barabara ya lami tabora hadi Mpanda, unategemea huo mkopo utalipwaje?
Evaluation ya mradi wowote hata kama unalipwa na serikali lazima watazame returns zake/faida kwa Taifa whether monitory or othermeans. Lazima ifanyike hivyo, huwezi kujenga kitu kisicho na faida na kujidai eti serikali inalipa, basi serikali hiyo ni ya vichaa.
 
Back
Top Bottom