Gazeti la The Economist: Rais Magufuli na CCM kuendelea kushika madaraka baada ya Uchaguzi Mkuu

Hili gazeti limetuharibia kabisa sisi wapinzani kwa wahisani wetu maana tuliwaaminisha kuwa tutashinda uchaguzi ujao kwa kishindo cha msingi watupe tu pesa kwa ajli ya maandalizi sasa sijui tutawashawishi vipi tena watuelewe. Tulisusia uchaguzi wa Serikali za mitaa ili wahisani wasije kujua kuwa sisi bado dhaifu na wasingetupatia pesa tena. Hakika hili ni pigo kwetu sisi wapinzani.
 
Weka sababu za Economist kwanini Magufuli atashinda, wacha kelele..

Au na wewe hapa unataka tujadili hisia za hao wazungu?!

Ziweke hapa halafu tuanze kuzijadili, kama ni positive au negative, but sio kukurupuka tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hata wakati ccm wako vizuri upinzani walipata viti vingi vya ubunge na kila uchaguzi wanaongezeka na hata this time kama chadema wakimsimamisha lissu take my word wabunge watakaa na wengi watarudi
 
Gazeti pia linatoa ujumbe kwa wapinzani kuwa wajiandae kwa ''mafuriko ya kisiasa''!
Nisilo elewa mimi na hii elimu yangu mangungu ni kuwa inakuwaje kwenye uhakika huo wa ushindi bado ccm inakosa confidence?
Haitaki kutoa nafasi sawa za kufanya siasa, imewaamuru Polisi kuwadhibiti wapinzani kila kona, haitaki Tume huru ya uchaguzi na mengineyo ya aina hiyo? Unauhakika wa ushindi inakuwaje uwahonge na kuwatisha marefa?
Nadhani hata hao wabobezi wa Economist wameliona hilo kuwa kwa vile hali ni hiyo basi hakuna namna lazima wajitangaze ushindi

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Mpaka hapa nilikuwa najiuliza nini hasa lengo la mleta mada kwa suala lililo wazi kabisa (obvious). Wenye interest na siasa za Tanzania hawana shaka kuwa hususan “Under the leadership of John Magufuli, the long-standing ruling party, the CCM, will retain a firm grip on power’’. Huhitaji utafiti wa haja wala kauli ya The Economist kujua hilo. Kwa EIU huo ni mteremko.

Na sidhani kama ni vyema kufurahia kauli ya aina hiyo iliyokaa kikejeli kejeli tena baada ya muda mrefu wa kubainisha uhasama kati ya gazeti hilo na serikali. Hivi kauli ya “a firm grip on power” imeeleweka ipasavyo? Is that something positive?
 
Sumu hailambwi kwa ulimi
 
T
The economist hawa wanafiki tu!
Sasa ndo wanajifanya kuanza kubalance story sio?
Too late, tulishawastukia siku nyingi sana. Maleongo yao na wanayemtumikia tunayajua hata mkijifanya leo mnakuwa neutral na kuanza kuuona ukweli.
 
Kwahiyo nawe umekubaliana na hili gazeti kwamba serikali ya Meko INA uwezo mdogo kifedha?

Mwenyewe (Meko) si ndiye amekuwa akituaminisha kwamba serikali yake ni ya kitajiri na kwamba nchi hii ina uwezo hata wa kutoa misaada kwa nchi nyingine!

Tukisema Meko kaharibu uchumi wetu mnapinga.
Hii nchi uchumi uko hoi tofauti na ilivyokuwa enzi za Kikwete na Mkapa.

Standard ya maisha ya watu inazidi kushuka kila iitwapo leo. Watanzania hawana uhakika hata wa milo miwili kwa kutwa.

Si watumishi wa umma, wafanyabiashara, wakulima, wamachinga na hata wavuvi wanaofurahia maisha, wote wamepigika. Leo nyanya moja inauzwa kwa sh. 500 lakini bado Meko na serikali yake ya kidhalimu wanataka kutuaminisha kwamba maisha ya watanzania ni mazuri.

Nakuhakikishia kwamba CCM na huyo dikteta wenu mtapata taabu sana kwenye kampeni za uchaguzi 2020. Sijui mtawaambia mini wananchi hawa waliopigika.
Wafikishie ujumbe wale wanaowaita mabeberu kuwa Gazeti la The Economist limeandika,‘’Under the leadership of John Magufuli, the long-standing ruling party, the CCM, will retain a firm grip on power’’.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
T

The economist hawa wanafiki tu!
Sasa ndo wanajifanya kuanza kubalance story sio?
Too late, tulishawastukia siku nyingi sana. Maleongo yao na wanayemtumikia tunayajua hata mkijifanya leo mnakuwa neutral na kuanza kuuona ukweli.
Ukweli UPI wameuona ambao hawaujui? Wanajua kila kitu kuhusu sisi. Na wanatujua kuliko tujijuavyo wenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ujinga sasa paschal Mayala

Wewe hiyo milele utakuwepo wewe utaishi milele change your Mind

Mtu unayeweza kudead hata baada ya leo unajuaje CCM itatawala milele



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo paragraph yako ya mwisho sio kweli. Watanzania wanakaribia milioni sitini halafu unadai unafikiri wapinzani hawana watu wa kuweza kuunda serikali.

Ina maana malioni woote hao ni ccm au wewe unafikiri chama kingine kikija madarakani ndio Civil Service yoote inaoondolewa.

Watanzania kwa kuwa ni chama kimoja tu ndicho kinatawala siku zote hamuelewi chama kingine kikishika dola hali inakuwaje, mnafikiri kitapashwa kutafuta hata watendaji kata na ma-das kutoka nje ya nchi. Very sorry.
 
Mkuu Pascal Mayalla huhitaji kuomba ruhusa lakini hata hivyo umeonyesha unyenyekevu kitaaluma kwa kuomba ruhusa!

Tumia utakavyo hasa kwa manufaa ya kuelimisha wajinga wa hapa Jamiiforums!
I believe wewe ndie mjinga namba moja kuleta vitu visivyo na sababu halafu unataka werevu wajadili, considering ulivyoisifia hiyo Intelligence Unit ya hao jamaa zako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…