Elias Msuya
Platinum Member
- Dec 23, 2011
- 267
- 1,014
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) imewataka madereva hao kupata mafunzo ili kuepuka madhara kwao na kwa watu wengine.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti wa GCLA, Daniel Ndiyo leo Julai 3, akisema dereva anayesafirisha kemikali bila kupata mafunzo anafanya kosa kisheria na akikamatwa atapigwa faini ya Sh500,000, huku kampuni iliyomwajiri nayo ikipigwa faini ya Sh2.5 milioni.
“Dereva hapaswi kusafirisha kemikali bila kupata mafunzo ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali. Kupitia mafunzo hayo, atapewa mbinu zote za kuepuka madhara ya kemikali anayosafirisha. Kwa hiyo ukiona dereva analalamika kupata madhara ya kemikali, ujue huyo hakupata mafunzo na tukimkamata adhabu yake ni faini ya Sh500,000 na akishindwa tunampeleka mahakamani.
“Pia kampuni anayofanyia kazi itapigwa faini ya Sh2.5 milioni.
Soma pia: Chukua Tahadhari unapopishana na Magari yanayobeba kemikali za sumu ikiwemo ya Sianidi inayotumika kuchenjulia dhahabu
Amesema kwa kuwa madereva mara nyingi wanakuwa safarini, mafunzo yao huwa ni ya siku mbili, ambazo atapata mbinu za msingi za kujiepusha na madhara ya kemikali yeye mwenyewe na kwa jamii inayomzunguka.
Mbali na madereva, Ndiyo amesema kampuni zinazosafirisha kemikali zinapaswa kuwa na mtaalamu atakayekuwa akiandaa mwongozo wa kemikali (material data sheet) inayosafirishwa na utaratibu wa kujilinda.
“Huo mwongozo utakaoandikwa kwa lugha inayoeleweka (Kiswhaili), unakuwa na maelezo ya kemikali inayosafirishwa, madhara yake na namna ya kujilinda na utabandikwa kwenye gari analosafirishia,” amesema.
Amesema dereva anapokuwa safarini, halazimiki kuvaa vifaa vya kujikinga, isipokuwa tu kama atakuwa kwenye mazingira hatarishi kama vile kemikali hiyo imetingishika na kufunguka kwenye kifungashio chake.
“Hapo dereva atatakiwa kuvaa barakoa na glavu ili asije kuivuta au kuigusa. Kwa hiyo dereva aliyepewa mafunzo hawezi kuathiriwa na kemikali.
“Kwa mfano tindikali ni kemikali ambayo ikigusa mwili inatabia ya kuunguza ngozi na kama itagusa macho mtu anakuwa kipofu. Ikiwa mtu atavuta mvuke wake, anaweza kuathirika mapafu, hivyo ni lazima kufuata maelekezo aliyopewa kwenye mafunzo.”
Hata hivyo, alisema kamikali zinaposafirishwa hufungashwa vizuri zisije zikafunguka wakati wote wa safari.