Geita: Akutwa amejinyonga ndani ya nyumba ya wageni inayomilikiwa na mumewe

Geita: Akutwa amejinyonga ndani ya nyumba ya wageni inayomilikiwa na mumewe

Huna uwezo wala akili ya kuelewa nilichoandika hapo kwa sababu mfululizo wa mauaji yanayoendelea hapa nchini hata huyasikii kwa sababu unayapaka mafuta kwa kutumia mgongo wa mfalme Yezabeli.

ni lini Tanzania na duniani hakujawahi kuwa na mauaji...tafuta namna nyingine ya kufanya siasa.
 
samurai wa CCM unayapaka haya mauaji mafuta kwa mgongo wa mfalme Yezabeli😁😁😁

hiyo ndio shida chief, ushanibatiza mimi CCM kwasababu nimewaza tofauti.... hahahaha.

sisi watoto wa kitaa haya ni mambo ya kawaida sana ya vifo, huko kanda ya ziwa vifo havijawahi kuwa maajabu tena vyakipumbavu kabisa...
 
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Naomi mkazi wa mji mdogo Katoro wilayani Geita mkoani hapa amekutwa amejinyonga kwa kamba ya manila ndani ya choo cha nyumba ya kulala wageni inayomilikiwa na mumewe.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema polisi wanaendelea na uchunguzi wa kifo hicho.

Tukio hilo limetokea Februari 3, 2022 saa 12 jioni baada ya mwanamke huyo kufika kwenye nyumba ya wageni na kumtaka mmoja wa wahudumu amsaidie mtoto mwenye umri wa miezi minne kwa kuwa yeye anajisikia vibaya.

Akizungumzia tukio hilo, mhudumu wa nyumba hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Monica Paul amesema, mke wa mwajiri wake alifika kwenye eneo hilo saa 8 mchana na kumtaka amsaidie mtoto ili yeye apumzikekwa kuwa hayuko vizuri kiafya.

Amesema baada ya hapo alipewa chumba, lakini baadaye walikuta mwili ukining’inia juu chooni, baada ya mteja mwingine kuomba huduma ya choo alichojinyongea mwanamke huyo.

Kiongozi wa eneo hilo, Stephano Bandola amesema hawajajua chanzo cha mwanamke huyo kujinyonga lakini akadai inaweza kuwa mgogoro wa kifamilia.

Juhudi za kumpata mume wa mwanamke huyo hazikufanikiwa baada ya kuelezwa yuko safarini nje ya Katoro.

MWANANCHI
Geita kwa wiki matukio ya mauaji hayapungui manne,bado shinyanga napo hayapungui manne
 
Back
Top Bottom