GEITA: Amteka mpenzi wake akitaka arudishiwe hela alizohonga, amuua

Bravo snr

Senior Member
Joined
Aug 16, 2020
Posts
182
Reaction score
477

Amteka mpenzi wake akitaka arudishiwe hela alizo honga, amuua​

WhatsApp-Image-2021-06-29-at-13.09.24-660x400.jpeg
Jeshi la Polisi Mkoani Geita linamshikilia mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 30 kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake aitwaye Esta John (28) mkazi wa Ibamba Wilaya Bukombe Mkoani humo ambaye kabla ya kifo chake alitekwa nyara na mpenzi wake.

Katika taarifa ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Henry Mwaibambe aliyoitoa kwa waandishi wa habari inasema kwamba mwanamke huyo aliondoka nyumbani kwake juni 13 mwaka huu akiwa na mtu aliyesemekana ni mpenzi wake.

Baada ya kutoweka kwa muda mwanaume huyo ambaye jeshi la polisi halijamtaja kwa majina yake, alianza kuwapigia simu wazazi wa mwanamke akihitaji kulipwa pesa alizokuwa akimuhudumia kwa ahadi ya kumuoa na kwamba mtuhumiwa alibaini kuwa sio mwaminifu.

Kamanda Mwaibambe amesema baada ya taarifa kufika katika vyombo vya usalama upelelezi ulianza mara moja na kufankiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa na mali za marehemu ambaye alimteka nyara.

“Katika mahojiano alikiri kumteka nyara mwanamke huyo akishinikiza kulipwa gharama alizotumia kumtunza kwa ahadi ya kuoana lakini alibaini kwamba sio mwaminifu, aliposhindwa kurudisha pesa yake ndipo alichukua uamuzi wa kumuua na kumzika huko katika kijiji Masota Wilaya ya Bukombe’’ Kamanda Mwaibambe.

Aidha amesema mtuhumiwa aliwaongoza Askari Polisi mpaka eneo alikomzika ambapo hatua za kisheria zilifuatwa ikiwmo kufukua kaburi na kufanya uchunguzi wa utambuzi wa mwili wa marehemu na kwamba uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea na upelelezi ukikamilia mtuhumiwa aafikishwa katika vyombo vya sheria.
 
Uamuzi wa kijinga sana huu,ndoa hailazimishwi,ndoa ni hisia,but mapenzi yanauma,kama mtu huna nia nae ni bora ukamwambia mapema ili kuepusha majanga kama haya,

Jamaa anaenda kuozea jela kisa makaratasi! bila shaka kwa muda huu anajutia sana maamuzi yake But it's too late,

Siku zote usichukue maamuzi ukiwa na hasira wala usitoe ahadi ukiwa na furaha.
 
Uamuzi wa kijinga sana huu,ndoa hailazimishwi,ndoa ni hisia,but mapenzi yanauma,kama mtu huna nia nae ni bora ukamwambia mapema ili kuepusha majanga kama haya...
Sijui kwanini watu ni washamba kiasi hiki yaani ugombane na mwanamke kisha umuuue!?? Hapana kama hanitaki na apite tuuu wapo wengi tuuu
 
Hivi mademu kwa nini wanapenda tu pesa lakini hawana uaminifu? ......demu unamthamini, tuseme unampa zawadi 5m. au unamnunulia ndinga ya kutembelea, baada ya mwezi tu nyodo zinaanza, hapo lazima wajiandae na maswahibu kama haya....
 
Amteka mpenzi wake akitaka arudishiwe hela alizo honga, amuua​

By
Pascal Mwakyoma
WhatsApp-Image-2021-06-29-at-13.09.24-660x400.jpeg

Jeshi la Polisi Mkoani Geita linamshikilia mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 30 kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake aitwaye Esta John (28) mkazi wa Ibamba Wilaya Bukombe Mkoani humo ambaye kabla ya kifo chake alitekwa nyara na mpenzi wake.

Katika taarifa ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Henry Mwaibambe aliyoitoa kwa waandishi wa habari inasema kwamba mwanamke huyo aliondoka nyumbani kwake juni 13 mwaka huu akiwa na mtu aliyesemekana ni mpenzi wake.

Baada ya kutoweka kwa muda mwanaume huyo ambaye jeshi la polisi halijamtaja kwa majina yake, alianza kuwapigia simu wazazi wa mwanamke akihitaji kulipwa pesa alizokuwa akimuhudumia kwa ahadi ya kumuoa na kwamba mtuhumiwa alibaini kuwa sio mwaminifu.

Kamanda Mwaibambe amesema baada ya taarifa kufika katika vyombo vya usalama upelelezi ulianza mara moja na kufankiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa na mali za marehemu ambaye alimteka nyara.

“Katika mahojiano alikiri kumteka nyara mwanamke huyo akishinikiza kulipwa gharama alizotumia kumtunza kwa ahadi ya kuoana lakini alibaini kwamba sio mwaminifu, aliposhindwa kurudisha pesa yake ndipo alichukua uamuzi wa kumuua na kumzika huko katika kijiji Masota Wilaya ya Bukombe’’ Kamanda Mwaibambe.

Aidha amesema mtuhumiwa aliwaongoza Askari Polisi mpaka eneo alikomzika ambapo hatua za kisheria zilifuatwa ikiwmo kufukua kaburi na kufanya uchunguzi wa utambuzi wa mwili wa marehemu na kwamba uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea na upelelezi ukikamilia mtuhumiwa aafikishwa katika vyombo vya sheria.
Mbona upelelezi umeshakamilika

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Polisi kata mko mnafanya nn kwenye mitaa/,vijiji ,kaziyenu nikutoa elimu kuzuia mauaji nahalifu mbalimbali au mnafanya kazi yakugonga wanawake tu.tumechoka na kupewa taarifa za mauaji
 
Back
Top Bottom