Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nchi Imeoza Sana Kama Mbolea Ya Mbojo (Wachache Watanielewa) Bado Tunapaka Mafuta Ukisema Huku Kuzuri Kule KubayaTena Kapteni Mstaafu wa JWTZ!
NASEMA Uongo Ndugu ZanguSafi sana wasomi watoNdiyo Ukweli Wenyewe
ke chato
Nenda kapimwe akili yako, Chato Ipo Geita. Unadhani mchango wa Geita kwa pato la Taifa ni mdogo?Unafananishaje Arusha /Mirerani na Chatto kwenye kuchangia pato la taifa?
Ni mbingu na ardhi.
Na kama unadhani CCM ilishinda kihalali basi unahitaji msaada wa tiba ya akili.
Naona aibu mimi!Tena Kapteni Mstaafu wa JWTZ!
Uzee huja na busara ila waqt mwingine uzee huja peke yakeUzee sio busara, hata wajinga wanazeeka pia[emoji445][emoji444][emoji445]
Kingewekwa mwanzaKampasi ya Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la kanda ya ziwa kitajengwa wilayani Chato, amethibitisha waziri wa utumishi wa umma George Mkuchika.
Kwa mujibu wa Mkuchika ni kuwa amejiridhisha kuwa Chato inazo sifa zote zinazoiwezesha kujenga chuo hicho ikiwemo ukubwa wa eneo unaoridhisha.
=======
TPSC KUJENGA KAMPASI CHATO KUKIDHI KIU KANDA YA ZIWA
CHUO cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kiko mbioni kujenga kampasi wilayani Chato, mkoani Geita itakayotoa fursa ya mafunzo kwa Watumishi wa Umma na wananchi wa Kanda ya Ziwa.
Akikagua eneo litakalojengwa Kampasi hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni mstaafu George Mkuchika alisema ameridhika na eneo lililotengwa kwani ni rafiki kwa usalama na utoaji wa elimu.
Kampasi itajengwa eneo la Rubambangwe lenye ekari 41.66 na itahudumia mikoa ya Geita, Mwanza, Kagera, Shinyanga, Simiyu na Mara.
Waziri Mkuchika alisema Kanda ya Ziwa pekee ndiyo ilikuwa haijabahatika kuwa na Kampasi ya Chuo cha Utumishi wa Umma, hivyo fursa hii ni muafaka na itakuwa na manufaa kwa watumishi wa umma na wakazi wa eneo la Kanda hiyo.
Akizungumzia uamuzi wa kujenga Kampasi hiyo wilayani Chato, Mkuchika alifafanua kuwa halmashauri ya wilaya ya Chato imetoa kiwanja hicho bure tofauti na maeneo mengine ya Kanda ya Ziwa ambayo yangekigharimu chuo fedha nyingi kununua kiwanja.
Aliishukuru halmashauri kwa kutoa kiwanja na kumhimiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato kuharakisha mchakato wa upatikanaji wa hati kwani chuo kiko tayari kuanza ujenzi mapema iwezekavyo.
Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dk Emmanuel Shindika aliwathibitishia wakazi wa Kanda ya Ziwa kuwa fedha za kuanza ujenzi zimeshapatikana, hivyo kinachosubirikiwa ni hati.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chato, ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Medard Kalemani alimtaka Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo kuwasilisha maombi ya kupatiwa umeme katika eneo hilo ili kuharakisha ukamilishaji wa ujenzi wa kampasi hiyo.
Akizungumzia eneo ambalo chuo kitajengwa, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel alisema ujenzi wa kampasi hiyo ukikamilika itakuwa ni chachu ya maendeleo kutokana na muingiliano wa watu kutoka maeneo mbalimbali watakaokuja kupata mafunzo na utavutia uwekezaji.