Geita Gold Fc 0-1 Yanga Sc | NBC PL | CCM Kirumba

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Ni mechi kubwa kwa wapenzi wa soka wa Kanda ya Ziwa. Geita Gold itakuwa inawakaribisha Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC katika Dimba la CCM Kirumba pale jijini Mwanza.

Geita imehamishia mchezo huu katika dimba hilo badala ya Nyankumbu ili kuongeza kipato. Kitendo hiko kimekemewa sana na mashabiki wa Geita.

Kocha Mkuu wa Geita, Fred Felix Minziro anasema timu yake iko vizuri wachezaji wana morali na mechi na leo wako tayari kupambana na kuvuna alama 3.

Yanga itaingia uwanjani ikimkosa Saido Ntibazonkiza aliyebaki Dar, huku winga Chico Ushindi naye akikosekana katika mchezo huu.

Mechi ni saa 10:00 jioni kupitia Azam Sports 1HD na updates zitakujia hapahapa, usikose kujumuika nasi...

======

Mpira umekwisha kwa Geita kukubali kichapo cha bao moja bila majibu kutoka kwa Young Africans, goli pekee la mchezo likifungwa na Fiston Mayele dakika ya kwanza.
 
Asante kwa ushauri tumepokea taarifa hizo na kwa bahati mbaya tunakutarifu uzi huu utakuwa wa Moto 🔥.

Ila Geita ikifungwa tunafuta uzi ila Geita ikishinda tuna ubana kabisa kwenye jukwaa hili na uwe special thread.

Asante
 
Wananchi Wa Mwanza Wana-Vibe La Kutosha Sana.


Congratulations Wananchi Mwaka Wetu Na Mwingine Mingi Inafata.
 
Kamisaa Wa Mchezo Wa Leo Pamoja Na Captains Wanapiga Picha Ya Pamoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…