Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Miaka nenda rudi kilio chetu kimekuwa ni uboreshwaji stendi yetu lakini hakuna kitu kinafanyika.
Kipindi cha mvua tumekuwa tukipata shida sana kwani hii stendi huwa inajaa maji na hata kupishana kwa magari huwa ni changamoto sana.
Sisi watu wa mabasi na wale madereva wanaoendesha mafuso tumekuwa tunapata shida hata kupishana vizuri barabarani.
Inafikia wakati, kipindi cha masika sisi madereva hatulali majumbani inatubidi tulale kwenye magari yetu maana tunaogopa magari yetu hapa stendi kumezwa na mafuriko.
Hali ni mbaya sana na tunaomba serikali itusaidie.
Hivi kweli Mkoa wa Geita ambako madini ya dhahabu yanatoka yanaenda Ulaya, tunakosaje kuwa na stendi ya kisasa?
Kama Serikali imeweza kutujengea barabara nzuri na za kisasa tunaamini kuwa hata hii stendi pia wanaweza kuiboresha.
Pia soma ~ Serikali Geita yatenga Bilioni 14 kukarabati na kujenga Stendi Kuu ya Mabasi