KERO Geita inatoka dhahabu lakini Stendi yetu ya Mabasi kama Kijiji kilichotelekezwa

KERO Geita inatoka dhahabu lakini Stendi yetu ya Mabasi kama Kijiji kilichotelekezwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mli



Mlilaumu lile shetani lenu la Chato badala ya kujenga Mkoani lenyewe likaenda kujenga kikijijini kwake!
Acha kumsingizia Magufuli!
Ni magufuli pekee ndiyo aliifufua Geita, toka enzi za uhuru Geita hakuwa na barabara ya lami ya mtaa hata moja hadi kipindi cha JPM

Ni sawa alipendelea Chato lakini aliikumbuka Geita kuliko awamu zote zilizowahi kupita wala iliyopo

Na angemaliza miaka yake hata hili bandiko lisingekuwa hapa!
 
Hali halisi iko hivi msilalamikie sana viongozi wengine viongozi na wananchi wa Geita nini mmejifanyia nyie wenyewe zaidi ya showoff. Viongozi walioko na waliopita wamefanya nini katika mji huo wanakuja na kuondoka kama wanakuja holiday.

Geita shule nzuri ni za private pale mjini barabara iko moja tu ya kuingia na kutoka Geita town wameiweka hadi traffic lights. Labda kuna sababu ya hili jambo.

Kuna matajiri wakubwa Geita wao wakishilikiana na GGM wanauwezo wa kusimamia hiyo Stand ijengwe na zile tax zina kusanywa. Hiyo ndio selfishness waliyo kuwepo nayo viongozi na wenye mji wao hawajali watu wa chini, wao wakishatoka na magari yao wewe kajamba nani ni shauri yako.

Geita kuna kujuana ndio maana kunabaki na kutabaki hivyo kama hawata badili hizo tabia zao (wananzengo) kujuana.

Kuna miji mingine haina utajiri wa Geita na wako mbali sana kimaendeleo. Uchaguzi unakuja wapate kujifuza yaliyo wapata na wawapige chini viongozi wote(wafanye clean up) na waweke sura mpya za kufanya kazi na mji utabadilika. Hayo ni maoni yangu tuu. Tanzania ni yetu sote hata Geita pia inaishi watanzania ndio maana inauma.
 
Back
Top Bottom