GE2025 Geita: Jimbo la Bukombe aliyechukua fomu ya ubunge ni Dkt. Dotto Biteko peke yake, majimbo mengine 102 wati nia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Wakati watia nia kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkoa wa Geita wakijitokeza kwa wingi kuchukua na kurejesha fomu za kuomba ridhaa ya kugombea ubunge, Jimbo la Bukombe limebaki na jina moja pekee—Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Doto Biteko, ambaye ameonesha nia ya kuendelea kulitumikia jimbo hilo.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Geita, Andrew Mnuke, jumla ya wanachama 102 wamejitokeza kuwania nafasi ya ubunge katika majimbo tisa ya mkoa huo. Hii ni dalili ya hamasa kubwa ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu ujao na kuendelea kuimarika kwa demokrasia ndani ya chama hicho tawala.

Soma Pia: Uzi maalum wa wanaotia nia kugombea Ubunge Uchaguzi Mkuu 2025

Majimbo na idadi ya watia nia waliopokea fomu ni kama ifuatavyo:

Chato Kaskazini – 15

Chato Kusini – 18

Busanda – 8

Katoro – 13

Geita Mjini – 18

Jimbo la Geita – 8

Mbogwe – 14

Nyang’hwale – 7

Bukombe – 1

Katika orodha hiyo, wanaume ni 85 na wanawake 17, jambo linaloashiria uhamasishaji unaoendelea kwa jinsia zote kushiriki kwenye uongozi wa taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mnuke amesema:

"Mwitikio huu mkubwa unaonyesha imani ya wanachama kwa chama chao na ari ya kushiriki kwenye mchakato wa demokrasia kuelekea uchaguzi mkuu. Hili ni jambo la kujivunia kama chama na kama mkoa."

Screenshot 2025-07-03 194911.png
 
Kalemani kwa nini anagombea? Hajafanya lolote
 
View attachment 3392937
Nizamu z Uoga ni jadi ya CCM
 
Na ndg yake anachukua jimbo jpya la katoro kiulaini kabsa BAHIMA EMPIRE IS REAL...
BAHIMA tena mkuu!!!!Hivi Kuna jimbo jipya la Katoro duuh...mbona hatari sana wameyabebanisha hivyo eneo karibu karibu. Geita majimbo 2....Katoro tena jipya duuh
 
Deupty PM anapita bila kupingwaa? Lol
Situlisema tumerekebisha sheria hamna kupita bila kupingwa rufaa yangu ipo njiani,na pia na jiandaa na kutupiliwa kwake mbali.
 
Kwa hiyo ataendelea kuwa deputy au ndo kaimaliza Mwendo?
 
Back
Top Bottom