Geita. Mjamzito auawa kikatili kwa kuchinjwa, wauaji nao wauawa

Geita. Mjamzito auawa kikatili kwa kuchinjwa, wauaji nao wauawa

Bravo AI

Senior Member
Joined
Jan 13, 2023
Posts
133
Reaction score
281
Geita. Mwanamke mwenye ujauzito wa miezi saba aliyetambuliwa kwa jina la Renata Elias (27), ameuawa kikatili na mtoto wake wa kambo kwa kuchinjwa shingo huku chanzo kikidaiwa kuwa ni mgogoro wa kifamilia na tamaa ya mali.

Tukio hilo lililotokea usiku wa Februari 17, 2023 linadaiwa kufanywa na vijana wawili ambapo mmoja ni mtoto wa mume wa mwanamke huyo na kwamba baada ya kufanya mauaji hayo nao waliuawa na wananchi wenye hasira kali.

Katika tukio hilo, pia baba wa familia hiyo aliyetajwa kwa jina la Msafiri Renatus alijeruhiwa kwa kuchomwa kisu ubavuni na kichwani na amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Geita kwa matibabu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kwamba aliyetekeleza tukio hilo la kinyama anaitwa Jackson Msafiri (25) ambaye alikuwa na rafiki yake.

Mkuu wa wilaya ya Geita, Cornel Magembe ameitembelea familia iliyoathirika na tukio hilo kulaani vikali huku akitoa pole kwa familia na kuwashukuru wananchi kwa kuonyesha umoja uliofanikisha kumnusuru Msafiri na kumwahisha hospitali baada ya kujeruhiwa.

“Sisi kama serikali tumefika kuwapa pole kwenye jambo hili zito na baya ambalo kwa binadamu yeyote mwenye akili anaona ni tukio baya la kufedhesha utu wa binadamu watu tunatofautiana kwenye kufikiri na kutenda.

“Kilichofanywa ni kitendo kibaya sana, niseme tu nawashukuru wananchi kwa kujitokeza mliposikia na ushirikiano huu uendelee ili kudhibiti matukio ya aina hii,” amesema Magembe.

Mihayo Renatus ambaye ni kaka mkubwa wa Msafiri, amezungumzia tukio hilo akisema majira ya saa 2 usiku, mtoto mkubwa wa Msafiri akiwa na kijana mwenzake walifika nyumbani na kugonga kisha kufunguliwa geti na kuingia ndani kuangalia TV na baada ya muda mfupi walitekeleza mauaji hayo baada ya mwanamke huyo kuingia bafuni kuoga.

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Safia Jongo hakupatikana kuzungumzia tukio hilo baada ya simu yake ya mkononi kutopokelewa.
 
Mzee hakumpa kijana wake usalama wa mali...
Huenda kijana yuko well aware walivyozitafuta pesa hizo kwa taabu labda na mama yake mzazi ila mzee kachukua binti anayelingana naye..

Who knows!!! Huenda huyu bi mdogo alimweka kati baba akawa boya na akajimilikisha mali zote..

Si bure..

Kuna somo hapa.
 
Mali hizi hizi tunazokaa nazo kwa miaka isiyozidi 90 huku tukiwa na uwezo wa kuzifurahia si zaidi ya miaka 70?!!!!!! Dunia ina miaka billion kadhaa tangu iundwe na hata haijulikani kuna miaka mingapi kabla ya kuisha.

Ikifikia eneo hili, napenda sana nasaha za dini ya Kiislamu ya kutoihangaikia kupitiliza dunia na kwa nasaha hizi wamefanikiwa sana kuepusha vitendo kama hivi maeneo yao!
 
Tafuta pesa zako acha kutegemea urithi,utakufa kibudu
Ndio hayo hayo yanatokea Kila siku,wazee kuoa uzeeni kabla hawajaoa wawape usalama wa Mali watoto,unakuta umri umekwenda wanalogwa na maslay queen wa mjini ,wanajisahau.

Watoto wa mengi Wana Mali zao lakini angalia wanavyo kimbizana mahakamani kwa ajili ya Mali ni hayo hayo sema uyo kijana hajatumia njia sahihi
 
Ndio hayo hayo yanatokea Kila siku,wazee kuoa uzeeni kabla hawajaoa wawape usalama wa Mali watoto,unakuta umri umekwenda wanalogwa na maslay queen wa mjini ,wanajisahau.watoto wa mengi Wana Mali zao lakini angalia wanavyo kimbizana mahakamani kwa ajili ya Mali,ni hayo hayo sema uyo kijana hajatumia njia sahihi
Labda huyo mzee mke wake wa kwanza amekufa, kwanini asioe tena wakati ana nguvu, au unataka aanze kuimba pambio la vijana wa hovyo, " KATAA NDOA"?
 
Back
Top Bottom