Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Waheshimiwe watoto wakambo mama huyo alitakiwa kuomba talaka endapo alihsi kijana huyo kwake nikizingiti ,sio kuaza kum-beza kwenye mambo muhimu ya familia ,wapendeni ndo hao panyaroad kitaaHebu fafanua vizuri
Wasiojulikana wamejaa sana kanda ya ziwa.Geita. Mwanamke mwenye ujauzito wa miezi saba aliyetambuliwa kwa jina la Renata Elias (27), ameuawa kikatili na mtoto wake wa kambo kwa kuchinjwa shingo huku chanzo kikidaiwa kuwa ni mgogoro wa kifamilia na tamaa ya mali.
Tukio hilo lililotokea usiku wa Februari 17, 2023 linadaiwa kufanywa na vijana wawili ambapo mmoja ni mtoto wa mume wa mwanamke huyo na kwamba baada ya kufanya mauaji hayo nao waliuawa na wananchi wenye hasira kali.
Katika tukio hilo, pia baba wa familia hiyo aliyetajwa kwa jina la Msafiri Renatus alijeruhiwa kwa kuchomwa kisu ubavuni na kichwani na amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Geita kwa matibabu.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kwamba aliyetekeleza tukio hilo la kinyama anaitwa Jackson Msafiri (25) ambaye alikuwa na rafiki yake.
Mkuu wa wilaya ya Geita, Cornel Magembe ameitembelea familia iliyoathirika na tukio hilo kulaani vikali huku akitoa pole kwa familia na kuwashukuru wananchi kwa kuonyesha umoja uliofanikisha kumnusuru Msafiri na kumwahisha hospitali baada ya kujeruhiwa.
“Sisi kama serikali tumefika kuwapa pole kwenye jambo hili zito na baya ambalo kwa binadamu yeyote mwenye akili anaona ni tukio baya la kufedhesha utu wa binadamu watu tunatofautiana kwenye kufikiri na kutenda.
“Kilichofanywa ni kitendo kibaya sana, niseme tu nawashukuru wananchi kwa kujitokeza mliposikia na ushirikiano huu uendelee ili kudhibiti matukio ya aina hii,” amesema Magembe.
Mihayo Renatus ambaye ni kaka mkubwa wa Msafiri, amezungumzia tukio hilo akisema majira ya saa 2 usiku, mtoto mkubwa wa Msafiri akiwa na kijana mwenzake walifika nyumbani na kugonga kisha kufunguliwa geti na kuingia ndani kuangalia TV na baada ya muda mfupi walitekeleza mauaji hayo baada ya mwanamke huyo kuingia bafuni kuoga.
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Safia Jongo hakupatikana kuzungumzia tukio hilo baada ya simu yake ya mkononi kutopokelewa.
mtoto tangu anamiaka 5 anachunga mifugo anafikisha miaka 30 babake anachukua sehemu ya mali hiyo kuolea mke mwingine unadhani matokeo yake nn?Geita. Mwanamke mwenye ujauzito wa miezi saba aliyetambuliwa kwa jina la Renata Elias (27), ameuawa kikatili na mtoto wake wa kambo kwa kuchinjwa shingo huku chanzo kikidaiwa kuwa ni mgogoro wa kifamilia na tamaa ya mali.
Tukio hilo lililotokea usiku wa Februari 17, 2023 linadaiwa kufanywa na vijana wawili ambapo mmoja ni mtoto wa mume wa mwanamke huyo na kwamba baada ya kufanya mauaji hayo nao waliuawa na wananchi wenye hasira kali.
Katika tukio hilo, pia baba wa familia hiyo aliyetajwa kwa jina la Msafiri Renatus alijeruhiwa kwa kuchomwa kisu ubavuni na kichwani na amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Geita kwa matibabu.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kwamba aliyetekeleza tukio hilo la kinyama anaitwa Jackson Msafiri (25) ambaye alikuwa na rafiki yake.
Mkuu wa wilaya ya Geita, Cornel Magembe ameitembelea familia iliyoathirika na tukio hilo kulaani vikali huku akitoa pole kwa familia na kuwashukuru wananchi kwa kuonyesha umoja uliofanikisha kumnusuru Msafiri na kumwahisha hospitali baada ya kujeruhiwa.
“Sisi kama serikali tumefika kuwapa pole kwenye jambo hili zito na baya ambalo kwa binadamu yeyote mwenye akili anaona ni tukio baya la kufedhesha utu wa binadamu watu tunatofautiana kwenye kufikiri na kutenda.
“Kilichofanywa ni kitendo kibaya sana, niseme tu nawashukuru wananchi kwa kujitokeza mliposikia na ushirikiano huu uendelee ili kudhibiti matukio ya aina hii,” amesema Magembe.
Mihayo Renatus ambaye ni kaka mkubwa wa Msafiri, amezungumzia tukio hilo akisema majira ya saa 2 usiku, mtoto mkubwa wa Msafiri akiwa na kijana mwenzake walifika nyumbani na kugonga kisha kufunguliwa geti na kuingia ndani kuangalia TV na baada ya muda mfupi walitekeleza mauaji hayo baada ya mwanamke huyo kuingia bafuni kuoga.
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Safia Jongo hakupatikana kuzungumzia tukio hilo baada ya simu yake ya mkononi kutopokelewa.
Hizi familia na tamaduni za ki-tz mambo huanzia mbali.Kijana miaka 25 Tamaa ya Mali ya Nini siutafute zako mbona mda unao mzuri
Ndivyo inavyokuwa wazazi wanatengeneza chukimtoto tangu anamiaka 5 anachunga mifugo anafikisha miaka 30 babake anachukua sehemu ya mali hiyo kuolea mke mwingine unadhani matokeo yake nn?
Kwahiyo unatakiwa uueMzee hakumpa kijana wake usalama wa mali...
Huenda kijana yuko well aware walivyozitafuta pesa hizo kwa taabu labda na mama yake mzazi ila mzee kachukua binti anayelingana naye..
Who knows!!! Huenda huyu bi mdogo alimweka kati baba akawa boya na akajimilikisha mali zote..
Si bure..
Kuna somo hapa.
Wazee wengine wako hovyo sana. Unakuta familia ina maisha magumu sana badala ajijenge kwanza anakimbilia kuoa.Labda huyo mzee mke wake wa kwanza amekufa, kwanini asioe tena wakati ana nguvu, au unataka aanze kuimba pambio la vijana wa hovyo, " KATAA NDOA"?
Madaraka ya Ubunge na Urais tu wa miaka mitano watu wanaalipuana Risasi na kubambikiziwa kesi za ubakaji mtu akaozee jela unazungumzia Mali za mtu maskini anazotegemea kukunja mkono kinywani??Mali hizi hizi tunazokaa nazo kwa miaka isiyozidi 90 huku tukiwa na uwezo wa kuzifurahia si zaidi ya miaka 70?!!!!!! Dunia ina miaka billion kadhaa tangu iundwe na hata haijulikani kuna miaka mingapi kabla ya kuisha.
Ikifikia eneo hili, napenda sana nasaha za dini ya Kiislamu ya kutoihangaikia kupitiliza dunia na kwa nasaha hizi wamefanikiwa sana kuepusha vitendo kama hivi maeneo yao!
Huenda leo ndo umekuja TZ ukitokea ng'ambo.Sio rahisi kusikia mambo ya kutisha ya aina hii yakitokea ukanda wa pwani, kuna ustaarabu mkubwa sana wa kuheshimu maisha pwani.
Umeongea point, sema kufikia kuua ni maamuzi yasio faa ila na sisi wazazi tujitafakari kuhusu mstakabari wa wanetu kuliko kujari nafasi zetu tuWazee wengine wako hovyo sana. Unakuta familia ina maisha magumu sana badala ajijenge kwanza anakimbilia kuoa.
Vijana wamekuwa kwa shida na hata kile kilichopo Baba anachukua kutoa mahari.
Sasa unakuta vijana hawamwezi baba wanakimbilia kwa wanayemuonea.
Ndo unafyeka watoto, wanawake!! Bado kuna namna nyingine ingeweza kufanyika zaidi ya kuchukua hizo nafsi.Madaraka ya Ubunge na Urais tu wa miaka mitano watu wanaalipuana Risasi na kubambikiziwa kesi za ubakaji mtu akaozee jela unazungumzia Mali za mtu maskini anazotegemea kukunja mkono kinywani??
Hii ni kutokana na gazeti la Mwananchi tarehe 18,2023Habari haijakamilika kabisa maana chanzo change cha taarifa kinasema vijana hao walikuwa wanne na walliua mama yao wa kambo & hosegirl