Geita: Mwanafunzi wa Kidato cha 2 auawa baada ya kutuhumiwa kuiba kuni kwenye Shamba la Miti

Geita: Mwanafunzi wa Kidato cha 2 auawa baada ya kutuhumiwa kuiba kuni kwenye Shamba la Miti

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Jesshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia Said Shabani (39) kwa kosa la kumuua Naomi James (17) mwanafunzi wa kidato cha pili, Shule ya Sekondari Kivukoni, mkazi wa Mtaa wa Nyatorotoro B, Kata ya Nyankumbu wilayani Geita Mkoani Geita kwa kumutuhumu kuiba kuni.

Akizungumza tukio hilo leo, Kamanda wa Polisi mkoani hapa (RPC) Henry Mwaibambe alisema tukio hilo lilitokea januari 18 mwaka huu katika msitu wa shamba la miti lililopo kata ya Nyankumbu ambapo marehemu alikuwa na wenzake wawili wakiwa wanatafuta kuni.

RPC Mwaibambe alisema wakati marehemu na wenzake wakiendelea kazi hiyo kwenye shamba linalomilikiwa na Said Shabani, ndipo mmiliki huyo alianza kuwakimbiza na bahati mbaya marehemu alianguka chini na kuanza kushambuliwa na mtuhumiwa kwa kitu chenye ncha kali na kusababisha kifo chake.
 
Hiyo kanda sijui watu wana roho gani
Kuua kwao siyo kesi kabisa
Kuna mijitu huko ina roho ya kishetani aise
Sasa unamuaa unachukua uhai wa binadam kisa
Kuni

Mazafyantaaaa

Ova
 
Back
Top Bottom