Katika hali ya kusikitisha, kadri tunavyozidi kukaribia uchaguzi mkuu, kumekuwepo na vitendo vya kihuni vya kutumia nguvu kupiga, kuumiza na kunyanyasa wananchi.
Katika mazingira yanayoonyesha kuwa matendo hayo si bahati mbaya, kumekuwepo na mfululizo wa kuvamia na kuharibu mali za wagombea wa Chadema katuka kile kinachoonekana ni vitendo vilivyoratibiwa.
Inavyoonekana, Wanufaika wa vitendo hivyo wameshaona kuwa hawakubaliki, wananchi wamewakataa, kwa hiyo waneamua kuleta fujo na vurugu ili kuwatisha wananchi wahofu kutumia haki yao ya kidemokrasia kujitokeza kwa wingi kupiga kura ya kuwakataa.
Pia vinalenga kuwaogopesha wagmbea wa upinzani, kuwatoa kwenye reli ili wasiconcentrate na kampeni bali wabaki na hofu ya maisha yao.
Siku za karibuni tumeona polisi wakijiingiza katika matendo ya kuonea na kusumbua wapinzani bila kosa lolote, hayo tumeyaoba huko Arusha, Tarime kwa Heche walipovamia ofisi na kuharibu vitu vya ofisi, Shinyanga walipojaribu kumbambikizia mbunge kosa la kuchana bango la Magufuli.
Huko Chato leo watu wasiojulikana wamevamia nyumba ya mgombea mbunge na kuichoma moto. Humo ndani kulikuwa na watoto, almanusra waungue wakiwa ndani.
Ninachotaka kuwaambia wahuni hawa ni kuwa, Hakuna fujo itakayorudisha nyuma maamuzi ya wananchi. Wananchi wameshawakataa, hawana tena kibali wala ridhaa ya kutawala, wanachoweza sasa ni kuchakachua tu lakini si kwa ridhaa ya wananchi.
Hii nchi imewahi kufanya chaguzi za vyama vingi lakini hatukuwahi kushuhudia kiwango cha utesi na ukatili tunaoushuhudia kwenye awamu hii ya tano. Ipo hsja kwa wananchi kuzuia ukatili wa kiwango hiki kabla hajujakomaa na hatimaye kutuletea shida huko mbeleni.
Hapa chini ni video ya nyumba ya mgombea ubunge wa Chadema huko Chato imepigwa kibiriti