Kuna mahali
Matola amezungumza maneno yenye uzito. Wapinzani hebu msomeni vizuri
Heshima ni two way traffic na wala Wapinzani wasidhani CCM na serikali na vyombo vyao hawajui haya
Msajili wa vyama anaona hatari ya kuunga mgombea wa chama kingine, haoni ya kuchomeana nyumba.
Laiti ingelikuwa Upinzani leo angeshinda katika vikao, barua na TV akifoka na kulaani.
Hili amekaa kimya, maana wanaotenda ni CCM ambao mwenyekiti wao ndiye mteuzi wake
Tume ya uchaguzi nayo kama Msajili ni kama vile hawaoni, nao pia M/kiti wa CCM ndiye amteuzi wao
Chadema wana matatizo. Haya mambo bila kuyaweka hadharani nchi na dunia ikayaona ipo siku mtakapojibu CCM na vyombo vyao wakapiga zumari mkaonekana ninyi ndio wabaya hata kama mnajitetea
Mbowe na Mnyika akina Husna ndio wenye jukumu? Ingalikuwa ACT Wazalendo reaction ingekuwa tofauti
Msajili wa vyama na NEC, Kenya ilianza hivi hivi !! Jiulizeni, uvumilivu ukiisha kwa wananchi mnaweza kuzuia gharika? Matasema nini? Kenya walikuwa na Jeshi na Polisi lakini nchi ilisambaratika. Hamjiulizi ilikuwaje?
Ninyi, NEC na Msajili,ninyi ndio wenye sheria hamuwezi kukwepa maswali,hoja wala kujitetea ikitokea dhoruba.Mtajificha nyuma ya CCM, ukweli ukitimia CCM watawakana mtasimama wenyewe!
Kivuitu wa Kenya alikuwa mtiifu, ilipotimia alisimama mwenyewe na kufariki katika dhalili kubwa sana
kwa msongo. Waliomtumia hawakumjua, hata familia yake haitaki kujihusisha na jina la Kivuitu.
Viongozi wa DINI, nanyi endeleeni kukaa kimya wala hakuna haja ya sala za kuliombea Taifa.
Endelezeni unafiki wenu bila kuwahusisha wananchi, waacheni wananchi na nchi yao
JokaKuu Pascal Mayalla (kada FYI)
Mag3 tindo