Geita: Polisi wakamata wawili tukio la mauaji ya kijana Enock

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Wakuu,

Jeshi la Polisi nchini Tanzania limetoa ufafanuzi kuhusu video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha kijana akiwa amefungwa mikono huku akipigwa kwa fimbo na watu kadhaa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 3 Julai 2025 na msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, tukio hilo lilitokea Juni 26, 2025, baada ya kijana huyo kushambuliwa na kundi la watu waliomtuhumu kuhusika katika mauaji. Kijana huyo aliyetambulika kwa jina la Enock Thomas Mhangwa alifariki dunia kufuatia kipigo hicho.

Soma,Pia: Kijana Enock Thomas Mhangwaock adaiwa kuuawa kikatili Msituni kwa kipigo kutoka kwa Watendaji wa vijiji vya Uyovu na Lyobahika

Taarifa hiyo imesema kuwa watuhumiwa wawili wamekamatwa wakihusishwa na mauaji hayo. Watuhumiwa hao wametajwa kuwa ni Ferdinand Antony, Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Liyobhaha, pamoja na Hussein Ally kutoka eneo la Madebe.

IMG_1602.jpeg
 
Safi sana hao watuhumiwa wakalionje joto la jiwe
 
Hiyo mikoa ya huko,inaonekana Ina idadi kubwa wananchi ambao kiasili sio watanzania!!

Kiuhalisia watanzania wengine hawana roho mbaya kama walioionyeaha hao jamaa!!
 
Uyo ndezi alievaa uzi wa Gunners akautoe.
 
Wakuu,

Jeshi la Polisi nchini Tanzania limetoa ufafanuzi kuhusu video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha kijana akiwa amefungwa mikono huku akipigwa kwa fimbo na watu kadhaa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 3 Julai 2025 na msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, tukio hilo lilitokea Juni 26, 2025, baada ya kijana huyo kushambuliwa na kundi la watu waliomtuhumu kuhusika katika mauaji. Kijana huyo aliyetambulika kwa jina la Enock Thomas Mhangwa alifariki dunia kufuatia kipigo hicho.

Soma,Pia: Kijana Enock Thomas Mhangwaock adaiwa kuuawa kikatili Msituni kwa kipigo kutoka kwa Watendaji wa vijiji vya Uyovu na Lyobahika

Taarifa hiyo imesema kuwa watuhumiwa wawili wamekamatwa wakihusishwa na mauaji hayo. Watuhumiwa hao wametajwa kuwa ni Ferdinand Antony, Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Liyobhaha, pamoja na Hussein Ally kutoka eneo la Madebe.

View attachment 3393128
Ndio magogo yale yale polisi wanayo tumia
 
Enock angekuwa mwanachadema, ingesemekana kapotea na hao jamaa kwenye picha ingesemekana hawajulikani
 
Back
Top Bottom