Geita: Serikali yashauri wazazi kutowanunulia simu watoto waliopo shuleni

Geita: Serikali yashauri wazazi kutowanunulia simu watoto waliopo shuleni

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Serikali ya Mkoa wa Geita imewataka wazazi mkoani humo kuacha kuwanunulia simu, Watoto wao ambao bado wapo mashuleni ili kuwaepusha na mmomonyoko wa madili unaotokana na mitandao ya kijamii.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita, Tito Mlelwa amesema “Jamii hasa wazazi wanatakiwa kubeba mzigo huo kwa kuwa wengi wao wanafanya hivyo ili kutaka kumfurahisha mtoto kwa kumpa kila kitu.”

Naye Chacha Wambura ambaye ni mzazi shuleni wa mwanafunzi, amesema simu zinawaharibu watoto wengi hasa wanapojiunga na makundi mbalimbali ya mitandao ya kijamii.

Chanzo: EATV
 
Hizo ni fikra za kizamani sasa hivi huwezi kutenganisha technology ya mawasiliano na hiki kizazi suala muhimu ni kila mzazi kusimamia mwanae tu.
 
Back
Top Bottom