carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Kwamba kumuua mwenzake siyo jinai? Kwa mtazamo wako.Nature inafanya kazi yake, sasa wanamfunga huyo Dogo kwanini?
Kumuua kwa kosa gani? Mapenzi? Si mnasema nature? Tena mwanaume kuwa dominant.Kwamba kumuua mwenzake siyo jinai? Kwa mtazamo wako.
Umeona mauaji tu?Nimeshalizungumzia suala la mauaji mikoa ya bara
Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia na kumhoji Lameck Isack, mhitimu wa Kidato cha nne mwaka 2026, kwa tuhuma za kumuua David Lucas, aliyekuwa mwenzake kwa kumchoma kwa kitu chenye ncha kali shingoni na ubavuni upande wa kulia.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari leo Ijumaa, Oktoba 30, 2026, na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo, tukio hilo lilitokea Alhamisi, Oktoba 29, 2026, saa 8 mchana Kijiji cha Mhama, Kata ya Namonge, Wilaya ya Bukombe, mkoani Geita.
Kamanda Jongo amesema kabla ya tukio hilo, mtuhumiwa, marehemu na vijana wengine watatu walikutana katika kijiwe kwa mazungumzo.Wote walikuwa wahitimu wa Kidato cha nne mwaka 2026 Shule ya Sekondari Said Nkumba.
Amesema muda mfupi baada ya kukutana, kulitokea mabishano kati ya mtuhumiwa na marehemu, ambayo yaligeuka ugomvi baada ya kila mmoja kudai kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msichana mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa.
Msichana huyo pia ni mhitimu wa Kidato cha nne katika shule hiyo.Katika ugomvi huo, mtuhumiwa anadaiwa kumchoma marehemu kwa kitu chenye ncha kali shingoni na ubavuni upande wa kulia, hali iliyosababisha kifo chake muda mfupi baadaye.
Kamanda Jongo ametaja wivu wa kimapenzi kuwa chanzo cha tukio hilo.Amesema mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi wa kitaalamu na kukabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya mazishi, huku polisi wakiendelea na uchunguzi ili mtuhumiwa afikishwe mahakamani.
Katika hatua nyingine, Kamanda Jongo ametoa wito kwa wazazi na walezi kuimarisha malezi, maadili na uangalizi wa watoto wao, ikiwemo kufuatilia makundi wanayoshirikiana nayo na kuwapa mwongozo na ushauri sahihi.
Chanzo : Mwananchi
MkuuHaya mauaji yamezidi sasa kwa wagalatia
Au ndio wanavyofundishwa huko makanisani ?
Naona ndio maandalizi
Tatizo ni shule waliyosoma inajina la kobaziHaya mauaji yamezidi sasa kwa wagalatia
Au ndio wanavyofundishwa huko makanisani ?
Naona ndio maandalizi
Wote walikuwa wahitimu wa Kidato cha nne mwaka 2026 Shule ya Sekondari Said Nkumba.
Unafki tu umewajaa.Mkuu
Labda nikusaidie Kidogo kukufumbua akili Macho na Kutoa Ujinga.
Ukristo Sio Dini.
Ukristo ni Imani thabiti ya Kumfuata na Kumuamini Yesu Kristo, kwa Kutenda Mema sawa sawa na Yesu alivyokuwa mwema au sawa sawa na Mafundisho yake.
Ukristo Sio Jina kama Pascal, Christopher
Lameck, Edward, Julius, Sarah, Christina victoria nk
Matendo ya Kikristo yesu au Mafundisho ya yake yalikuwa ni kutenda wema.
Mfano
43 Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;
Mathayo
lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
Mathayo 5:44.
USICHANGANYE MASHETANI WENYE DHAMBI, WAPAGANI, VUGUVUGU NA IMANI YA WAKRISTO.TENA ALISEMA UKIWA VUGUVUGU ATAKUTAPIKA.
Kwanini Nape hakuendelea na ile project ya robots pengine ingepunguza hii shidaJeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia na kumhoji Lameck Isack, mhitimu wa Kidato cha nne mwaka 2026, kwa tuhuma za kumuua David Lucas, aliyekuwa mwenzake kwa kumchoma kwa kitu chenye ncha kali shingoni na ubavuni upande wa kulia.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari leo Ijumaa, Oktoba 30, 2026, na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo, tukio hilo lilitokea Alhamisi, Oktoba 29, 2026, saa 8 mchana Kijiji cha Mhama, Kata ya Namonge, Wilaya ya Bukombe, mkoani Geita.
Kamanda Jongo amesema kabla ya tukio hilo, mtuhumiwa, marehemu na vijana wengine watatu walikutana katika kijiwe kwa mazungumzo.Wote walikuwa wahitimu wa Kidato cha nne mwaka 2026 Shule ya Sekondari Said Nkumba.
Amesema muda mfupi baada ya kukutana, kulitokea mabishano kati ya mtuhumiwa na marehemu, ambayo yaligeuka ugomvi baada ya kila mmoja kudai kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msichana mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa.
Msichana huyo pia ni mhitimu wa Kidato cha nne katika shule hiyo.Katika ugomvi huo, mtuhumiwa anadaiwa kumchoma marehemu kwa kitu chenye ncha kali shingoni na ubavuni upande wa kulia, hali iliyosababisha kifo chake muda mfupi baadaye.
Kamanda Jongo ametaja wivu wa kimapenzi kuwa chanzo cha tukio hilo.Amesema mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi wa kitaalamu na kukabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya mazishi, huku polisi wakiendelea na uchunguzi ili mtuhumiwa afikishwe mahakamani.
Katika hatua nyingine, Kamanda Jongo ametoa wito kwa wazazi na walezi kuimarisha malezi, maadili na uangalizi wa watoto wao, ikiwemo kufuatilia makundi wanayoshirikiana nayo na kuwapa mwongozo na ushauri sahihi.
Chanzo : Mwananchi
Hapa mgalatia Yoda huwezi kumuona.Haya mauaji yamezidi sasa kwa wagalatia
Au ndio wanavyofundishwa huko makanisani ?
Naona ndio maandalizi
Majina siyo utambulisho wa dini, kuna waislamu wengi wana hayo majina, wapo wakristo wengi wanatumia majina ya kiislam lakini bado maisha yanakwendaUnafki tu umewajaa.
Matendo hayo wakifanya watu wanaofanania na majina ya kiislamu moja kwa moja mnayahusisha na dini yake ila wakifanya wenye majina ya kikristo mnawatoa kwenye dini yao.