Black Butterfly
Senior Member
- Aug 31, 2022
- 130
- 368
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela amekabidhi magari matatu mapya kwa Wakuu wa Wilaya ya Geita, Mbogwe na Nyang’hwale yenye thamani ya zaidi ya Tsh. milioni 840.
Akikabidhi magari hayo katika Kata ya Bombambili Halmashauri ya Mji wa Geita, Shigela amewataka Wakuu wa Wilaya kuyatumia vizuri magari hayo ambayo yamenunuliwa kwa fedha za Serikali sambamba na kuwataka Madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani.
“Shukrani kwa Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo ameendelea kuwezesha mazingira ya Wafanyakazi na Ofisi ya Viongozi ambao wana jukumu la kumsaidia katika ngazi za Wilaya na Mkoa, tunamshukuru sana Mh. Rais kwa sababu fedha ambazo zimeletwa zaidi ya Tsh. milioni 840 ni fedha nyingi ambazo Mh. Rais ameona kuna haja ya kuleta fedha tununue magari”
Shigela amesema Wakuu wa Wilaya walikuwa wakihangaika kupata usafiri wa kwenda kutatua kero za Wananchi na kusema magari hayo yatakuwa mkombozi kwa Viongozi hao.
MillardAyoUPDATES