Geita: Wakuu wa Wilaya wapewa Magari 3 mapya yaliyogharimu Tsh. Milioni 840

Bajeti ya magari ya viongozi na viburudisho vya viongozi ni kubwa kuliko ya baadhi ya wizara muhimu zinazogusa maisha ya Watanzania wengi. Hii tu inatosha kukupa taswira juu ya taifa tulilonalo; na jamii tunayojaribu kuijenga!

SAD 😭




 
Upuuzi sana,halafu raia wanyonge ambao hata pair mbili za yeboyebo hawawezi miliki wanabebeshwa Kodi mara kununua umeme anakatwa,mara mia tatu simu.Hivi mls800 utakata 300 kwa watu wangapi. Je serikali ingeamua kubana matumizi mf gari isiwe juu ya ml45.
 
Sielewi kwanini mkuu wa wilaya ya kinondoni hatumii rav4
 
Mkoa mmoja tu, unakuta wakuu wa wilaya wanatumia 840m kwa magari tu, je uki-extraplotate nchi nzima ni pesa kiasi gani inaunguzwa kwenye magari tu- zaidi ya 20b. Halafu magari hayo hununuliwa karibu kila baada mwaka mmoja, yaani baada ya miaka miwili au mitatu, ma DC hao hao watapata magari mengine mapya bila kuuliza yale ya zamani yalikwenda wapi.
 
Mama yenu alielekeza kula urefu wa kamba sasa wanakula kote kote
 
Inasikitisha sana, Mtanzania wa kawaida hayajui haya. Yeye bora kala mlo mmoja, kalala basi. Kila siku nasema humu, kuanzia kodi, mikataba na mikopo vyote hivyo, ni kwaajili ya maisha yao ya anasa. Wala si kwa maisha ya Mtanzania. Ushahidi huo hapo!
 
Na hayo watauziwa kwa madai ya kupunguza gharama za matumizi.
GenZ waanzishe mradi wa kukodiwa kusaidia wanaosinzia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…