GEITA: Wananchi wavamia kituo Cha Polisi, wawili wauawa

GEITA: Wananchi wavamia kituo Cha Polisi, wawili wauawa

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
6,944
Reaction score
14,351
Vijana wawili wamefariki dunia hii leo Septemba 11, 2024 baada ya wananchi 800 kuvamia na kufanya vurugu katika kituo cha polisi Lulembela wilayani Mbogwe mkoani Geita vurugu zilizoanzia katika eneo la mnada wa Lulembela baada ya watu wawili kuonekana wakiwa wamebeba watoto wawili na wananchi waliokuwa katika mnada huo kuwahisi kuwa ni wezi wa watoto na kuanza kuwashambuilia, ndipo akatokea Mtendaji wa Kata akawabeba kwenye pikipiki na kuwakimbiza katika kituo cha Polisi Lulembela.

Ambapo baada ya watu hao kufikishwa katika kituo cha polisi, wananchi hao walifika katika kituo hicho na kuwataka askari polisi wawakabidhi watuhumiwa hao ili wawaue na Askari walijaribu kuwaelimisha na kuwaeleza ni kosa na si vizuri kujichukulia sheria mkononi lakini walikaidi na baada ya askari kuona hali hiyo ya kuhatarisha maisha ya watu na mali za serikali walitumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya watu hao na iliposhindikana walitumia silaha za moto kwa kupiga risasi juu ili watu hao watawanyike

"Mbali na kushambulia kituo hicho kwa mawe na kutaka kuingia kwa nguvu ndani ya kituo hicho, wananchi hao walichoma moto gari moja lenye namba za usajili T.440 ATW aina ya Toyota Cardina lililokuwa limeegeshwa nje ya kituo hicho na katika vurugu hizo watu wawili wamepoteza maisha, mmoja ni mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 18 hadi 20 na wa pili ni msichana aitwaye Teresia John mwenye umri wa miaka 18, mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Lulembela ambaye nyumba yao inatazamana na kituo hicho cha Polisi," imeeleza taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini

Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa, "Hata hivyo, ilibainika kuwa watu waliokuwa wamebeba watoto hao ni Emanuel John (33) mkazi wa Kigamboni Lulembela ambaye alikuwa amembeba mtoto wake aitwaye Ikram Emanuel mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi na moja na wa pili anaitwa Ng'amba Leonard (24) ambaye alikuwa amembeba mtoto aitwaye John Emanuel mwenye umri wa miaka miwili na miezi nane, Mama wa watoto hao aitwaye Rachel Luhende (22) amethibitisha kuwa watoto hao ni wakwake na walikuwa kwa wifi yake ambapo baba yao mzazi na mjomba wao walikwenda kuwachukua,".

#EastAfricaRadio

FB_IMG_1726082211869.jpg
 
Back
Top Bottom