Geita yakubali kuundwa Mkoa wa Chato; Kakonko, Biharamulo na Ngara kumegwa. Sengerema kwenda Geita..

Naunga mkono kabisa kuundwa kwa mkoa wa Chato kwa sababu kuu moja, ... nayo ni kuisogeza serikali karibu zaidi na ukanda huu uliopakana na chanzo kikuu cha migogoro ya nchi za maziwa makuu (TUTSI/HUTU conflict zone)!
šŸ‘Š šŸ˜ŽāœŒļøšŸ’„ā˜ ļøā˜ ļøā˜ ļøšŸ’€
 
Wenyewe hawajaomba
 
Ujinga tu kupoteza muda kulalamika kukatwa au kutokatwa eneo. Hizi ramani wazungu walikata hadi kuwa na tanganyika hatukupiga kelele au kwa kuwa tulikuwa nyani na wazungu ni watu?

Nashangaa hata kwanini kibaha isiwe Dar, fikiria mtu anatoka Mukuranga anapita Dar kwenda mkoani kwake kwa shughuli za kiofisi huko kibaha Mkoani.

Zanzibar ni kama mkoa mmoja au miwili leo watu wanataka eneo lisikatwe ubaki mkoa wenye eneo kuuuubwa ni kuchelewesha huduma kuwa karibu na watu.

Labda ingeleta Mashiko kama tungejadili kwa mkutadha wa kuongezeka gharama kwa serkali maana watahitajika watumishi kwa mkoa mpya na wilaya zake.
 
Nijuavyo Mimi maamuzi hufanywa na mabaraza ya madiwani na Si DCC wala RCC. Hizi ni Kamati za kushauri tu ambazo hubariki au kushauri maamuzi ya mabaraza ya Madiwani. Aidha, zoezi hili ngumu na tata ni lazima lipate Baraka za wananchi. Hivyo lazima kiwe na Muhtasari ya Mkutano mikuu ya vijiji/mitaa yote Wilaya zitakazohama na zile zitakaosalia. Kwa Maelezo tunayosoma, nibkwamba mikoa yote athirika Mwanza, KAGERA, Kigoma, na Geita lazima ifanye vikao. Gharama hizi zote za nini? Faida ake ni zipi
 
He!!! Kumbe haijikidhi wanaomba wilaya kutoka mikoa mingine!!!! Ukistaajabu ya Musa...!!!!
 
Yes!!! Ne yeye apendelee Zanzibar!!!!
 
Ha ha ha!!! Porini Dom mama hapataki!!!! This is great!
 
N geita je?
 
Buriani Geita. Ni ushamba kuna ulazima gani? Mbona Morogoro haigawiki?
Well said, Morogoro tu mbona na. Mkoa wa Tabora nao ni mkubwa sana hatujawahi kusikia mapendekezo ya kuigawa mikoa hiyo - ukiangalia kwa umakini utaguduwa Mikoa mipya iliyo anzishishwa ilitokana na shinikizo la kisiasa za Mawaziri wakuu na baadhi ya mawaziri kutoka mikoa husika,mfano: Mkoa was Manyara,Mkoa wa Katavi, Mkoa wa Geita huyo huyo ndie muhusika mkuu wa kalazimisha uundwaji wa Mkoa wa Chato/Rubondo - mambo gani haya?

Kinacho shangaza zaidi we Mkuu wa Mkoa wa Geita ana interest gani katika uundaji wa Mkoa wa Chato, kama sio kwamba kuna ushinikizaji wa chini chini for some strange reasons ambazo hazina tija kwa Taifa zaidi ya ubinafsi tu uliyo pitiliza mipaka - ushinikizaji wa uundwaji wa Mkoa wa Chato mama Samia hasiuwekee maanani hata kidogo
 
Hivi uwingi wa mamikoa unaleta maendeleo kwa wananchi? Bongo bahati mbaya sana , yaani hatuna vipaumbele kabisa ni mawazo ya kuongeza vyeo tu na madaraka lakini tija kwa wananchi hatujadili kabisaaa
 
Mmeiba kura hamjatosheka mmeamua kuiba na ardhi ili mumfurahishe fudengešŸ˜‡
 
Chato ni mkoa ambao hautakuwa na mvuto kabisa.
Harafu wanataka kuipotezea radha kagera kwa kuitolea wilaya zake.
Hivi kwa nini wasikate mikoa mikubwa wanaenda kukata mkoa mdogo? Yaani hii nchi tumepigwa kabisa
Tabora ni eneo kubwa balaa, hebu wapeni mkoa mpya.
 
Mama Samoa huu utopolo piga chini kabisa,yule sadist tayari keshaanza kuliwa na mchwa unahofia nini
 
Kuendeleza ukabila wa Magufuli.
Yule alikuwa si mtu mzuri sana.
Upendeleo wa dhhiri.
Mama Samia akiingia mtego huu, basi kila Rais ajaye atataka kuweka mkoa hata kijiji chake.
 
Kashindwa nani kupiga U-Turn? Hivi amuoni yaliyo kumba mji aliozaliwa Mobutu Sseseko - hivi sasa zahama hizo ndio zimeanza kunyemelea mji Chato ambao alizaliwa JPM

Dunia haishangazwi na hilo kwa kuwa Mobutu na JPM wote walikuwa na hulka zinazo randana sana,walikuwa hawataki kukosolewa, walilazimisha kauli zao ziwe final bila kujali athali zinazo weza kusababishwa na baadhi ya mahumuzi yao ya kupendelea wazi wazi Wilaya/Majimbo yao kwa kutumia tax payers money big time kujenga mega infrastructure wilaya/kijiji waliko zaliwa bila aibu!!

Tujaribu kuwa wakweli hapa, upendeleo/blatant nepotism is unethical,Viongozi wetu wa kitaifa wanapashwa kukemea vitendo hivyo kwa nguvu zao zote na ingekuwa vizuri zaidi kama Bunge lingepitisha sheria ya ku- impeach Rais yoyote aliyepo madarakani akionekana anapendelea kupeleka maendeleo yaliyo pitiliza mipaka jimboni mwake,kupendelea ndugu zake na kabila lake - upendeleo huu unarudisha nyuma umoja wa Kitaifa.

Mbona hatukuwahi kushuhudia matendo haya ya ajabu wakati wa Uongozi wa: Baba wa Taifa,Mzee Mwinyi,MzeeMkapa na JPM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…