15 February 2025
Kivu DR Congo
JENERALI SULTANI MAKENGA AJITOKEZA HADHARANI, NA KUSISITIZA NIDHAMU
Jenerali Sultani Emmanuel Makenga ajitokeza na kutembelea askari waliotekwa wa jeshi la serikali la FARDC ambao, sasa wanapewa mafunzo ya kuondoa nidhamu mbaya waliyokuzwa nayo wakitumikia jeshi la serikali ya DR Congo. Akiongea kwa kiSwahili safi cha ofisa mkuu wa juu wa M23 alisema yafuatayo :
View: https://m.youtube.com/watch?v=kPaCzBr0FL4
Jenerali Sultani Emmanuel Makenga ambaye ni Army Chief of Staff ( Mnadhimu Mkuu wa Jeshi ) wa jeshi la muungano AFC/ M23 amewaasa askari hao wa FARDC kujifunza kwa bidii mafunzo watakayopewa na wakufunzi wa kijeshi wa M23
Jenerali Makenga akawauliza mateka hao kama wanapata chakula cha kutosha kutoka kwa askari wa M23 wakajibu, ndiyo afande tunapata chakula.
Jenerali Makenga amesema jeshi zuri ni lile lenye nidhamu, na kuwa wale walitotayari kuacha kuiba, kunyanyasa raia na kuvuta bangi walipokuwa FARDC waseme hapa hapa kuwa wapo tayari kuwa Jeshi la Wananchi lenye nidhamu, mateka wakajibu ndiyo afande.
Jenerali Makenga akasema mafunzo hayo ni kutoa ujinga wa jeshi la FARDC katika bongo zao ili wawe askari wazuri, wakuweza kuzingatia mafunzo ya wakufunzi wa kijeshi wa M23 ambao ni ndugu zao wakongomani.
Jenerali Sultani Emmanuel Makenga akasema baada ya wanajeshi hao wa FARDC walio mateka kumaliza mafunzo wataingizwa katika jeshi la M23 watapewa buti, soksi na uniform kupelekwa unit tofauti tofauti za M23 kumuondoa Felix Tshisekedi.
More info :
AFC = l’Armée Révolutionnaire Congolaise (ARC)
M23 = March 23 2009
Jina la M23 linatokana na kushindwa kwa mchakato wa mazungumzo kati ya CNDP na serikali ya Kongo tarehe 23 Machi 2009.