Pre GE2025 Gen Z hatushindwi kitu: Kampeni ya kukataa machawa na viongozi wabovu inaanza rasmi

Pre GE2025 Gen Z hatushindwi kitu: Kampeni ya kukataa machawa na viongozi wabovu inaanza rasmi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Keamba mmeamua kujipiga risasi masikiini? Maana hizo tabia zimekuja na hiyo tabia ilikuwemo kwa generations nyingi lakini ilikuwa ni miongoni mwa tabia za aibu sawa na ushoga na usagaji.
Ni wakati wa hii generation yenu ndiyo tabia hii imeonekana kuwa siri ya mafanikio, ndiyo mtaji ndiyo tabia ambayo inaipa CCM jeuri ya kufanya inavyojisikia. Hii ni tabia yenu hiyo ndiyo identity ya generation yenu.
😂😂😂 Mkuu bwana, uchawa haujifichi ujue, yaani umefukuta koteee ukaona hii ndio angle ya kitokea?!

#KataaMachawa
#KataaUozo2025
 
Nimekutana na post muda si mrefu kuhusu Mwijaku, nimefikiria tuanzishe kampeni hii ya kumaliza uchawa nchini na kuondoa viongozi wote ambao hawatufai. kama mtoa mada yule alivyoelekeza;

Kusoma post yake pitia hapa, tusIpoteze muda na kujaza server kueleza upya alichopost 👉 Mwijaku anajikuta nani hasa? Ifike mahala tuanze gomea biashara za chawa wote, unfollow kwenye mambo yao yote!

Twende kwenye mambo ya kufanya;

1. Kwanza unfollow chawa wote, mpaka kwenye page zao za biashara, wauza vipodozi, vyakula, wanamuziki, chawa, unfollow wote. Page zao ziko public, ni cha kufanya ni kupita mara kwa mara kwenye kurasa zao, kila wanachopost achia hashtag #KataaMachawa au #KataaChawa. Kwa viongozi chawa nao fanya hivyo hivyo, pitisha hashtag kwenye post zao zote. Tuna chawa wanaotetea ujinga humu acha hashtag kwenye post zao zote.

2. Kwa viongozi mafisadi, waiba pesa za umma kila siku wanatajwa kwenye ripoti za CAG hatuoni wakifungwa wala kufilisiwa na wale wanaokubali tufungiwe mitandao tutumie hashtag hii - #KataaUozo2025. Wote tunawajua viongozi mizigo, tunawajua mafisadi, tunawajua waotaka kutuzimia mtandao, tunawajua wabunge sehemu zote ambapo toka wachaguliwe hawaonekani tena jimboni, na hujawahi kumuona hata sikumoja akifungua mdomo kuwasemea wananchi wake, tembeza # hii kwenye kila post wanayoweka.

Usidharau mbinu hizi, tunaweza kurudisha discipline nchini waelewe wenye nguvu ni wananchi.

Kumbuka hashtag ni mbili tu #KataaMachawa na #KataaUozo2025

Hatuwezi kushindwa kwenye hili, kumbuka unampigania mama yako, baba, dada na kaka kaka zako, wadogo zako, ndugu na jamaa, na zaidi na the most important thing ni kuwa you are fighting for yourself!

LETS DO THIS!
Nitakuwepo
 
Sasa sijui machawa yatajificha wapi . Sasa yanaanza pigwa kama ngoma

#kataa machawa ,kunguni,viroboto.
# kataa na zika ccm.
 
Mtu na akili zako timamu utamfatiliaje mtu kama mwijaku,baba level kitenge na hao wasanii wote bongo
Yaani hao ndy wanakuhamasishaa kufanya jambo fulani wakitumwa na serikali ......
Mtu yoyote anaye wafatilia hawa
Basi kichwani mwake hamnazo

Ova
 
Pumba tupu, Hakuna watu wa ovyo kwenye hii nchi kama hao Gen Z
 
Kwamba mmeamua kujipiga risasi masikioni? Maana hizo tabia zimekuja na hiyo tabia ilikuwemo kwa generations nyingi lakini ilikuwa ni miongoni mwa tabia za aibu sawa na ushoga na usagaji.
Ni wakati wa hii generation yenu ndiyo tabia hii imeonekana kuwa siri ya mafanikio, ndiyo mtaji ndiyo tabia ambayo inaipa CCM jeuri ya kufanya inavyojisikia. Hii ni tabia yenu hiyo ndiyo identity ya generation yenu.
#kataa chawaa
 
Tanzania inahitaji GEN Z wakali zaidi ya Kenya
 
Dada yenu nawaunga mikono yote miwili. Tena naomba michawa ya humu, ikileta habari yoyote. Ni kuwawekea hashtags tu, msichangie chochote, mpaka waache uhayawani wao.
#kataamachawa
#kataaufisadi
#kataaccm
Exactly,ni hashtag tuu zitembee
 
Back
Top Bottom