Gen Z wa Tanzania wapewe ajira maana ukosefu wa ajira ni chanzo cha maandamano tunayoshuhudia Kenya na sasa Uganda

Kwani shule ulienda kusomea ujinga?

Mwili na na fikra za binadam hupata uzoefu kwa kutenda siyo kuwaza tu.
 
Wanajitahidi vitisho na drama zao kuogopesha. Wasubiri vijana wetu wamejifunza Bangladesh
Hujatishwa unaogopa, je ukitishwa?

Mnajidanganya sana akili zenu, kafufueni mashamba ya babu zenu siyo mnarundikana mijini tu. Mambo yapo kwa Bashe.
 
Unashangaa nini na "umri" ni namba tu?

Badala ya kushangaa shangaa kanunuwe karanga uchemshe na chumvi uuze mitaani, ujipatie uzoefu wa biashara.

Kumbuka; nimetaja karanga kama kigezo tu, inaweza kuwa chochote.
 
Badala ya kukazana na teua tengua ya vigogo, hizo nguvu zingetumika kuwaajiri vijana.
Vinginevyo, hizo hela mnazozifuja hamtazila wala kuzitumia kwa amani.
hiyo serikali itaajiri vijana wangapi katika nchi hii?
 
Tembelea mkoa wa Pwani uone viwanda vipya, kila sehemu.

Kwani sekta binafsi lazima uajiriwe, kwanini hujiajiri wewe mwenyewe?

SG
Akijiajiri mwenyewe hawezi kujiongoza, kujitawala na hana ubunifu wa kujiwekea Mikakati ya baadaye. Anataka aajiriwe halafu ajipumzikie(Atege kazi) lakini awe active sana kudai mshahara tena kwa nguvu.
 
hiyo serikali itaajiri vijana wangapi katika nchi hii?
Yeah. Idadi ya vijana waliopo na wenye sifa stahiki kuajiriwa serikalini ni kubwa sana i.e. ni wengi mno kuzidi idadi ya nafasi za ajira zilizopo/zinazopatikana. Kwa hiyo LAZIMA watakuwepo tuu watakaokosa ajira Serikalini. Lakini ajira kama ajira, zimejaa tele na hazijatoshelezwa.
Hili vijana hawalikubali na wakiambiwa wajiajiri -sekta binafsi hususan ktk kilimo wanang'ang'ania mijini.
 
Ni ukweli kabisa 👆 👆 japo mchungu - unauma..Watakapozinduka watakuta imeenda hiyo.
 
Waliandaliwa kuto kuhoji, endapo maandamano yakitokea jibu lake ni madhara ya kuto kuhoji na kuto sikilizwa, (silent society), the question is how long should people keep silent
 
Tembelea www.ajira.go.tz
Hakuna nchi iliyo ajili Wananchi wote
Ipo.
Kwa mfano nchi ya Tanzania (Popn. 62mil.+ )hakuna Mwananchi yeyote anayeshindwa kupata riziki yake ya kila siku kama akijishughulisha. Kumbuka na Kuzingatia kwamba hatupati mahitaji yetu(Riziki zetu)ss Watanzania kwa kupewa na Serikali; HAKUNA- Huo ndo ukweli halisi. Usidanganywe na kikundi cha wachache sana wanaosema eti wamesoma na wanataka waajiriwe na Serikali - wameshasahau kwamba hawakuwekeana Mkataba na Serikali kwamba akimaliza masomo Serikali itamwajiri. Wakiambiwa wajiajiri Sekta binafsi wanatishia kuandamana eti wao ni Gen. Z. Kwa maneno mengine ni kwamba Ajira ya Gen.Z waliojipa wao wenyewe ni kulalamika, kuitishia Serikali kwamba wataandamana na kuwaghilibu (kushawishi/kudanganya) vijana wenzao ambao wanajishughulisha ili wawaunge mkono kwenye ujinga huo.
Wanadhani ajira zipo tuu ila Serikali kwa kiburi na ukatili inawanyima.
Wakitangaziwa Ajira za siri huko Urussi, Israeli, Ukraine, Palestina, Wagner PMC, N. Korea wanazuga eti hawajaziona. Ni watata kwel-kweli hawa jamaa wanaojnasibisha kuwa Gen. Z. Sifa za Gen.Z zipo ila sio za hawa waBongo.
Dah! Wanashindwa basi hata kujiajiri kwenye ile Sekta inayopigwa vita na Mh. RC na hivi karibuni wanategemea kulamba 36 mil. chap.
 
Waliandaliwa kuto kuhoji, endapo maandamano yakitokea jibu lake ni madhara ya kuto kuhoji na kuto sikilizwa, (silent society), the question is how long should people keep silent
U go while the going is good.
 
Taka taka izi kaandamane mwenyewe na ujinga wenu
 
Maisha ya uhakika ni ya kujihangaikia, serikali inatengeneza mazingira ya kiuchumi lakini kujiajiri ni ubunifu wa mtu binafsi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…