Gen Z wabisha hodi Uganda

Gen Z wabisha hodi Uganda

Ninaiheshimu nguvu ya umma siwezi kuibeza ila kwa hao wa Uganda wana chembechembe kama za Watanzania hasa tawala mbili na katiba mbovu mbovu.

Kenya katiba yao rais sio mtu wa mwisho kila maamuzi anaweza kupingwa na mahakama au bunge.

Mfano juzi Ruto aliunda kamati ya kukagua deni la serikali huku akimuweka mjumbe rais wa chama cha wanasheria .

Chama cha wanasheria kikatoka na barua na kusema rais hatoshiriki na ni kinyume na katiba bali jukumu hilo aachiwe mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali .

Hata wale vijana waliokamtwa maandamano ya June 25 , jopo la wanasheria kutoka chama hicho kilikuwa na mchakato wa kuwatoa kizuizini na waliachiwa sababu walikuwa wakitekeleza haki yao kikatiba.


Ukija Tanzania mtu anapotea siku 29 polisi wanasema hawajui alipo ,mtu alitekwa Dar kapelekwa Arusha baadae katupwa Katavi porini ila polisi wanasema bado wanachunguza je wanachunguza kitu gani hasa?

Jana Samia kasema anafurahi kuona polisi wanatekeleza "maagizo" yake ! je maagizo hayo ni yapi yeye anatakiwa awekewe mipaka sio kuingilia kila kitu.

Uganda Museveni kampa mwanae ukuu wa majeshi , mkewe ni waziri .

Rwanda jana wamefanya igizo lao kwa jina la uchaguzi wakati mshindi anajulikana.

Hivyo basi Uganda ,Tanzania ,Rwanda ugonjwa wao mmoja hizi nchi zikipata katiba mpya basi biashara imekwisha.
Hili jambo la kuburuzwa na watawala linaumiza sana hizi nchi zetu.
 
Inaonekana hata umri wa kati nao wanamawazo kama ya GEN-Z, hii ina maanisha kwamba muda wowote walioko madarakani na katika kundi la wanasiasa (political class) watafurushwa na umma mkubwa kupitia nguvu ya umma people's power

ANGALIZO KUTOKA RIKA LA KATI, KUHUSU WENYE MAMLAKA KUZIBA MASIKIO YAO

View: https://m.youtube.com/watch?v=TeWDerrx2Hw

Kwanza hakuna bunge kuna genge la matapeli tupu
 
My take serikali yetu kama inakopa hela benki ya NMB kununua mabasi 100 kumnufaisha mwekezaji wa UDART , mda NI mwalimu ya Kenya na Uganda naona inayahitaji.
Aisee...
Em ngoja tuone.

Inasikitisha.
 
Inaonekana hata umri wa kati nao wanamawazo kama ya GEN-Z, hii ina maanisha kwamba muda wowote walioko madarakani na katika kundi la wanasiasa (political class) watafurushwa na umma mkubwa kupitia nguvu ya umma people's power

ANGALIZO KUTOKA RIKA LA KATI, KUHUSU WENYE MAMLAKA KUZIBA MASIKIO YAO

View: https://m.youtube.com/watch?v=TeWDerrx2Hw

Soon tutaongea lugha moja, one day hawa political hawatoamini jamii itakapo amka
 
Back
Top Bottom