Gen Z wabisha hodi Uganda

Gen Z wabisha hodi Uganda

Bongo ni simba na yanga tu

USSR
Magazeti bila kurasa za mbele kuchombeza simba na yanga hayauzi.

Hakuna kijiwe, yaani hakuna kijiwe cha kuuza magazeti kinachoongelea siasa.

Kila asubuhi utakuta watu wazima, vijana kwa watoto wakiumiza vichwa ni kwa jinsi gani Gamondi atapanga kikosi, nani ataanza kati ya Chama na Azizi Ki.
 
Nasikia vijana tayari kuna group huko whatsap limeanzishwa linaitwa lost generation limeanza kuratibu kila kitu na kuweka wazi kero na kashifa zinazohusu setikali ya mama kama ni kweli mama asikilize watu anaowaongoza zaidi ya hapo anaweza kupata shida
Asikilize vipi wakati alikwisha sema yeye ni 'chura kiziwi', hivi nyinyi watu wengine akili zenu huwa mnazipeleka wapi?
 
16 Julai 2024
Nairobi, Kenya

GEN-Z WAZIDI KUDINDA NCHINI KENYA

Wamejitokeza leo jumanne tarehe 16 Julai 2024 kuweka mbinyo wa kutaka mabadiliko ya kweli


View: https://m.youtube.com/watch?v=5oOf76eYUZE

GSU (FFU) inachukua hatamu huko Mlolongo huku maandamano yakianza kwenye Barabara ya Mombasa​

Magari yaliyokuwa yakisafiri kutoka Mombasa hadi Nairobi yalielekezwa kwa Expressway kwa muda​

Kwa ufupi
  • Vijana hao awali walivamia Barabara kuu ya Nairobi - Mombasa ambayo huwa na shughuli nyingi na kuiwekea vizuizi kabla ya kuwasha moto.
  • Kisha waliwashirikisha maafisa hao katika mapigano kabla ya GSU kuingia.

by GEORGE OWITIMwandishi wa habari

Habari
16 Julai 2024 - 15:00
Soma E-Karatasi
Maafisa wa polisi wakiwatawanya vijana waliokuwa wakiandamana baada ya kufunga barabara kuu ya Nairobi - Mombasa katika eneo la Mlolongo kaunti ya Machakos mnamo Julai 16, 2024.
Maafisa wa polisi wakiwatawanya vijana waliokuwa wakiandamana baada ya kuziba Barabara kuu ya Nairobi - Mombasa eneo la Mlolongo kaunti ya Machakos mnamo Julai 16, 2024 Picha: GEORGE OWITI
Maafisa wa Kitengo cha Huduma kwa Jumla wamehamia kuzima maandamano huko Mlolongo, Kaunti ya Machakos.
Kitengo hicho kilijiunga na vikundi vingine vya polisi katika operesheni ndani ya mji huo baada ya mamia ya vijana kumiminika mitaani katika maandamano ya kuipinga serikali siku ya Jumanne.
Vijana hao awali walivamia Barabara kuu ya Nairobi - Mombasa ambayo huwa na shughuli nyingi na kuiwekea vizuizi kabla ya kuwasha moto.
Kisha waliwashirikisha maafisa hao katika mapigano kabla ya GSU kuingia.
Magari yote yaliyokuwa yakisafiri kutoka Mombasa hadi Nairobi yalielekezwa kwa Expressway kwa muda kabla ya maafisa hao kuwarudisha nyuma vijana waliokuwa wakiongezeka.
Maafisa wa polisi wakiwatawanya vijana waliokuwa wakiandamana baada ya kufunga barabara kuu ya Nairobi - Mombasa katika eneo la Mlolongo kaunti ya Machakos mnamo Julai 16, 2024.
Maafisa wa polisi wakiwatawanya vijana waliokuwa wakiandamana baada ya kuziba Barabara kuu ya Nairobi - Mombasa eneo la Mlolongo kaunti ya Machakos mnamo Julai 16, 2024 Picha: GEORGE OWITI

Kikosi cha askari polisi kimesambazwa katika mji wa Mlolongo na viunga vyake.
Wenye magari wamekaa nje ya barabara kuu huku wafanyabiashara wote wakifunga maduka.
Vijana, hata hivyo, wako kote mjini huku wengine wakicheza michezo ya kujificha na kutafuta na maafisa ambao wamekesha.

Kukodisha mabomu ya machozi imekuwa mtindo tangu maandamano yalipoanza katika mji wa Mlolongo.
Miji ya jirani kama vile Athi River na Kitengela pia biashara zimefungwa.
 
GenZ wa Rwanda ghafla itakuwa GenZ wa Kihutu wanazunguka na Mapanga kuwasaka GenZ wa Kitutsi.

Itachukua muda mrefu kuondoa hayo mambo na Kagame so far ameanza kufanikiwa.
Rwanda naambiwa mtaani watu wanaogopa kumkosoa huyo dikteta hata mtaani ukisikika tu unapotezwa.
 
GenZ wa Rwanda ghafla itakuwa GenZ wa Kihutu wanazunguka na Mapanga kuwasaka GenZ wa Kitutsi.

Itachukua muda mrefu kuondoa hayo mambo na Kagame so far ameanza kufanikiwa. Mwezi uliopita nilikuwa Kigali wahutu na watusi hawapendani kabisa wanachukiana kimyakimya wanaita inzigo
 
Mwezi uliopita nilikuwa Kigali wahutu na watusi hawapendani kabisa wanachukiana kimyakimya wanaita inzigo

Ukabila utaondolewa Rwanda aliyepanda Ukabila ni Wakoloni wa Kibelgiji na lengo lao lilikuwa ni Devide and Rule.
 
Hiyo movement naona itafika Ghana,Nigeria etc nao wameshaeka tareh yakuandamana tiari
 
Inaonekana hata umri wa kati nao wanamawazo kama ya GEN-Z, hii ina maanisha kwamba muda wowote walioko madarakani na katika kundi la wanasiasa (political class) watafurushwa na umma mkubwa kupitia nguvu ya umma people's power
Wakati sisi CHADEMA tunaandamana maandamano ya AMANI wengi wa Wafanyabiashara walikuwa wanatubeza sasa wanakomeshwa wanaanza kulialia.

Maandamano ya AMANI ya CHADEMA yajayo sijui kama watayabeza tena.😁
 
Back
Top Bottom